TGDC Tanzania

TGDC Tanzania TGDC is responsible for spearheading the development of geothermal resources in Tanzania.

07/03/2026

Kuelekea siku ya wanawake duniani, Jenipher Tillya, Mkaguzi wa ndani- TGDC,alikuwa na ujumbe huu.

06/03/2026

Kuelekea siku ya wanawake duniani, Khadija Ahmed, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, alikuwa na ujumbe huu.

05/03/2026

Kuelekea siku ya wanawake duniani, Judith Gowelle, Meneja Rasilimali watu na Utawala alikuwa na ujumbe huu.

Katibu Mkuu Nishati anayeshughilikia Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Felchesmi Mramba leo Machi 04, 2026 Amekutana na Kam...
04/03/2026

Katibu Mkuu Nishati anayeshughilikia Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Felchesmi Mramba leo Machi 04, 2026 Amekutana na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) kupata taarifa za Maendeleo ya Miradi ya Jotoardhi katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Innocent Luoga, Mkurugenzi wa Mipango na Sera Wizara ya Nishati Bw. Petro Lyatuu pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wizarani. Na kwa upande mwingine TGDC iliwakilishwa na Meneja Mkuu Mha. Mathew Mwangomba aliambatana na Uongozi wa Kampuni pamoja maafisa waandamizi.

Kikao hicho kililenga utoaji wa taarifa ya maendeleo ya Miradi Jotoardhi, hususan mradi wa kipaumbele wa Ngozi na pia kuimarisha usimamizi, uwazi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya TGDC ili kuimarisha Uendelezaji wa Miradi ya Jotoardhi nchini.

04/03/2026

Kuelekea siku ya wanawake duniani, Monica Komba, Meneja Fedha - TGDC, alikuwa na ujumbe huu.

03/03/2026

Kuelekea siku ya wanawake duniani, Mha. Esther Range, Mhandisi Mazingira Mwandamizi alikuwa na ujumbe huu.

Siku ya pili ya kikao kazi cha TGDC kinachofanyika siku ya leo 24 Feb 2026, Arusha.
24/02/2026

Siku ya pili ya kikao kazi cha TGDC kinachofanyika siku ya leo 24 Feb 2026, Arusha.

24/02/2026

Siku ya pili ya kikao kazi cha TGDC kinachofanyika siku ya leo 24 Feb 2026, Arusha.

Matukio mbalimbali katika Kikao kazi cha TGDC kinachofanyika siku ya leo 23 Feb 2026, Arusha.
23/02/2026

Matukio mbalimbali katika Kikao kazi cha TGDC kinachofanyika siku ya leo 23 Feb 2026, Arusha.

23/02/2026

Matukio mbalimbali katika Kikao kazi cha TGDC kinachofanyika siku ya leo 23 Feb 2026, Arusha.

TGDC na Chuo cha Ufundi Arusha Wasaini Mkataba wa Mashirikiano.Arusha, Februari 20, 2026 — Tanzania Geothermal Developme...
20/02/2026

TGDC na Chuo cha Ufundi Arusha Wasaini Mkataba wa Mashirikiano.

Arusha, Februari 20, 2026 — Tanzania Geothermal Development Company Limited (TGDC) na Arusha Technical College (ATC) leo wamesaini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding – MoU) yenye lengo la kuimarisha ujenzi wa uwezo (capacity building) na ushirikiano wa kitaaluma katika sekta ya jotoardhi na fani zinazohusiana na teknolojia na uhandisi.

Makubaliano hayo yalisainiwa katika viwanja vya Chuo cha Ufundi Arusha, jijini Arusha, ambapo TGDC iliwakilishwa na Meneja Mkuu, Eng. Mathew Mwangomba, huku ATC ikiwakilishwa na Profesa M***a Chacha.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Eng. Mwangomba alisema ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kukuza rasilimali watu wenye ujuzi wa kitaalamu katika sekta ya jotoardhi, sambamba na kutoa fursa za mafunzo kwa wanafunzi na wahadhiri wa chuo hicho.

Kwa upande wake, Profesa Chacha alisema MoU hiyo itafungua milango ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa vitendo (industrial training), tafiti za pamoja, ubadilishanaji wa wataalamu, pamoja na kuandaa programu za mafunzo zitakazokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Ushirikiano huu unatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha sekta ya nishati jadidifu nchini, kukuza ubunifu, na kuwajengea vijana ujuzi unaohitajika katika maendeleo ya viwanda na uchumi wa taifa.

Ramadan Kareem
19/02/2026

Ramadan Kareem

Address

Ursino Road
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TGDC Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category