07/04/2023
Katika miaka million 250 hadi miaka million 66 iliyopita dunia ilipita katika kipindi kinajulikana k**a Mesozoic Era, katika kipindi hiki dunia ilikua haitawaliwi na binadamu tena bali ni kipindi kilichotawaliwa na viumbe wakubwa wajulikanao k**a Dinosaurs.
Hichi kipindi kilikua kipindi cha ajabu sana katika historia ya dunia maana kulikua na wanyama wakubwa sana, mfano: hata Mijusi unayoiona hii leo enzi izo ilikua ina umbo kubwa labda k**a umbo la kulingana na mamba, Vyura walikua wakubwa kupindukia, pamoja na wanyama wengine wengi na hii wanasayansi wanasema ilisababishwa na dunia kipindi hicho kuwa na mimea mingi na Oxygen kubwa sana na k**a inavyojulikana kisayansi, mwili ukipata Oxygen nyingi hukua kwa wingi.
Wanasayansi wanasema kwamba katika kipindi hiki licha ya kuwa na wanyama wakubwa na kutisha bado viumbe wa jamii yetu sisi binadamu waitwao mamalia bado waliweza kuishi lakini kutokana na viumbe wakubwa na hatari waliotawala dunia kwa kipindi hicho ilipelekea hawa mamalia waweze kujificha kwenye mashimo kwa kipindi kirefu cha maisha yao, na hali hii ya kujificha kwenye mashimo iliwasaidia sana siku ya kiama ilipofika....
Moja kati ya nadharia inayoaminika zaidi ya kiama cha Dinosaurs ni ile inayoitwa (K-Pg) inayosema kwamba kuna kimondo kikubwa sana kutoka angani kilidondoka na kuangamiza zaidi ya asilimia 75 ya viumbe vyote duniani pamoja na miti kwa kipindi hicho na hii ni baada ya ule mtikisiko uliosababishwa na kimondo icho kusababisha mito mkubwa, volcano, Tsunami, Matetemeko na kadhalika. Baada ya Dinosaurs wote kuangamizwa pamoja na viumbe wale wakubwa na hatari kuangamizwa hiyo sasa ndio ikawa mwanya wa wale viumbe wadogo Mamalia kutoka katika mashimo waliokua wamejificha ndani yake na kuanza kuitwala dunia, kulingana na wanasayansi wanavyosema; Binadamu alitokana na jamii ya hawa mamalia baada ya Dinosaurs kuangamizwa walitoka na kuanza kuitawala dunia kwa mamilion ya miaka na waliendelea kubadilika kutokana na kupitia mabadiliko mbalimbali ya kisayansi.
Kuna vithibitisho vingi sana vya uwepo wa Dinosaurs duniani mfano: Baadhi ya mifupa ya Dinosaurs, Meno yao, Mayai na kadhalika
Like, share and comment.