Tanzania Yetu Kikwetu Kwetu

Tanzania Yetu Kikwetu Kwetu Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tanzania Yetu Kikwetu Kwetu, Biotechnology company, Dar es Salaam.

28/02/2015

Pumzika kwa Amani Captain Komba. Mbele yetu Nyuma yako. CCM italiona pengo lako daima.

Asante wadau wa zao la pamba Mnsotokea mikoa yote inayolima zao la pamba. Kwa pamoja tutafika.
23/02/2015

Asante wadau wa zao la pamba Mnsotokea mikoa yote inayolima zao la pamba. Kwa pamoja tutafika.

16/02/2015

Uthubutu ni sifa kuu ya Kiongozi. Watanzania wamechoshwa na Rushwa tutaiondoa kwa umoja wetu. Maamuzi sahihi yafanyike katika kuwachagua viongozi wetu.

Tanzania Imara inajengwa na Watanzania wenye viongozi imara.
14/02/2015

Tanzania Imara inajengwa na Watanzania wenye viongozi imara.

13/02/2015

Wakati nikitafakari juu ya hali ngumu ya wakulima katika nchi na namna gani watakuwa tabaka lenye thamani, wengine Wanawaza juu ya mavazi.

Ninawaomba Watanzania wenzangu tufikie wakati tutazame Kiongozi mwadilifu, Mzalendo, mchapakazi na anaeweka maslahi ya Taifa mbele na sio kujilimbikizia Mali na kuvaa nguo nzuri.

Tanzania inahitaji Mabadiliko ya kweli 2015.

KWA WATANZANIA WOTE SALAAM...NAPENDA KUWASHUKURU WALE WOTE WALIOJUMUIKA NAMI KWA AJILI YA KUSHEREHEKEA SIKU YA KRISMASS ...
27/12/2014

KWA WATANZANIA WOTE SALAAM...

NAPENDA KUWASHUKURU WALE WOTE WALIOJUMUIKA NAMI KWA AJILI YA KUSHEREHEKEA SIKU YA KRISMASS

HAKIKA MMEONESHA UPENDO WA DHATI NA NAOMBA TUENDELEE NA MOYO HUO

PIA NACHUKUA FURSA HII KUWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WATANZANIA WENZANGU WOTE POPOTE PALE DUNIANI

ASANTENI & HAPPY NEW YEAR 2015.

25/10/2014

HABARI ZA JUMAMOSI
NDUGU ZANGU TUNAELEKEA KATIKA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA NAWAOMBENI SANA TUJITAHIDI KUWAPIMA NA KUCHAGUA VIONGOZI WAADILIFU ,WANAOJITUMA,NA WENYE UTASHI WA KISIASA KWA AJILI YA MAENDELEO YA WATU NA TAIFA

WAKATI UMEFIKA KWA WATANZANIA KUONDOKANA NA MFUMO WA KUUZA MALIGHAFI KATIKA MASOKOimagesNA SULEIMAN MSUYAWAZIRI wa Nchi ...
24/08/2014

WAKATI UMEFIKA KWA WATANZANIA KUONDOKANA NA MFUMO WA KUUZA MALIGHAFI KATIKA MASOKO
images
NA SULEIMAN MSUYA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Mipango Stephen Wassira amesema wakati umefika kwa Watanzania kuondokana na mfumo wa kuuza malighafi katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili waweze kupata faida kubwa ya mazao wanayozalisha.
Wassira alisema hayo wakati alipohudhuria Mkutano wa Bodi ya Magavana ya Proffensial Trade Association (PTA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa miaka mingi wakulima wa Tanzania wamekuwa wakiuza malighafi badala ya bidhaa iliyokamilika kutokana na malighafi hiyo hali ambayo inachangia wanyonywe na wanunuzi.
Waziri huyo wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Mipango alisema ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mabadiliko kutokana na kilimo Serikali inaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha kuwa viwanda vinakuwepo katika maeneo ya wakulima .
“Kilimo ni moja ya sekta nzuri sana ila huwezi kuona manufaa yake iwapo wewe kila siku unauza malighafi kwa wenzako waliondelea jambo ambalo wanahakikisha kuwa linakwisha”’ alisema.
Wassira alisema Serikali inaendelea kutafuta wawekezaji ambao watakuja kuwekeza na kuwa kichochoe cha kukuza uchumi wa wakulima na jamii kwa ujumla.

Aidha alizungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia Benki ya PTA kwa Tanzania ambapo alisema kuwa imetoa msaada wa uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam, Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere.
Waziri Wassira alisema serikali itaendelea kushirikiana na benki hiyo ya maendeleo ya PTA ili kuhakikisha kuwa inaendeleza sekta mbalimbali hasa kupitia mpango wa pili wa maendeleo ambao unatarajiwa kuaanza hivi karibuni.

Huyu Ndiye Stephen Masato Wasira Aliyesoma Balili Shule Ya Msingi,Na Kisangwa Middle School Wilayani Bunda◄Stephen Masat...
03/08/2014

Huyu Ndiye Stephen Masato Wasira Aliyesoma Balili Shule Ya Msingi,Na Kisangwa Middle School Wilayani Bunda◄

Stephen Masato Wasira alizaliwa mwaka 1945 Wilayani Bunda,Mkoa wa Mara,Akiwa mdogo Stephen M.Wasira alisoma Elimu yake ya Msingi Shule ya Msingi Balili na Kisangwa Middle School, Wilaya ya Bunda, baada ya hapo aliendelea na masomo yake ya Sekondari katika Shule ya British Tutorial College.

Aliendelea na Masomo ya ngazi ya juu nchini Marekani huko alipata kusoma shahada Tatu za Uchumi na Utawala.Alisoma Shahada ya Kwanza katika Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa,Shahada ya Uzamili katika Uchumi na Shada ya Uzamili katika Utawala, zote kutoka Chuo Kikuu cha Amerika (American University) Jijini Washngton D.C.

Katika Maendeleo yake k**a Mtumishi wa Umma,Wasira alipata kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali,Kwanza; aligombea na Kushinda kuwa Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mwaka 1970 hadi 1975. Katika kipindi hiki cha Mwanzo k**a Mbunge aliteuliwa na Mwalimu Julius K.Nyerere kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Mwaka 1975,Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara,alikuwa katika nafasi hiyo tangu mwaka 1975 hadi 1982 alipoteuliwa kuwa Waziri na Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Washington,D.C.
Mwaka 1985,baada ya kutoka Marekani,aligombea na kushinda kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda kwa miaka mitano,Katika kipindi hiki aliteuliwa na Rais Ali H. Mwinyi kuwa Naibu Waziri wa Serikali za Mitaa, na baadae akawa Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo mwaka 1989 hadi 1990.

Mwaka 1990, Wasira aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani nafasi aliyoitumikia mpaka mwaka 1991, na baadae Mwaka 1995 aligombea na Kushinda Jimbo la Bunda akiwa k**a Mbunge wa Upinzani, hakutumikia nafasi hiyo kwa kipindi chote mpaka 1996 alipoondolewa katika nafasi hiyo.

Takribani Miaka kumi alijielekeza katika Biashara yaKampuni yake iitwayo Siza Cold Storage Ldt iliyokuwa ikisafirisha nje ya nchi mazo yatokanayo na bahari.Mwaka 2005 alirudi tena Bungeni kupitia Jimbo la Bunda nafasi aliyopita bila kupingwa,ameendelea kuwakilisha Jimbo hilo kwa kipindi chote hadi Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuongoza jimbo hilo.

Chini ya Uongozi wa Rais Jakaya M.Kikwete, Mhe.Wasira ametumikia Wizara tatu,Kwanza; aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji January hadi October 2006. Baada ya hapo aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika mpaka 2010, Pia aliweza kutumikia kwa muda Ofisi ya Waziri Mkuu k**a Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa(TAMISEMI) February hadi May 2008. Baada ya Uchaguzi Mkuu October 2010,Mhe.Wasira aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu,nafasi anayoendelea kuitumikia mpaka sasa.

Ndani ya Chama Tawala,Chama Cha Mapinduzi, amekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu miongoni mwa wajumbe 370(NEC) chombo cha juu kabisa cha maamuzi na sera za Chama,Amekuwa katika nafasi hii tangu 2007. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwaMjumbe wa Kamati Kuu miongoni mwa wajumbe 28 , baadae alichaguliwa tena katika nafasi hiyo February 2013. Mnamo November 2012 alichaguliwa kwa kishindo kuwaMjumbe wa Halmashauri Kuu kwa kipindi kingine cha Miaka mitano.

Mhe. Wassira atakuwa katika mdahalo mkubwa utakaofanyika siku ya Jumapili kuanzia saa 9.00 Alasili mpaka saa 12. 00 jion...
25/07/2014

Mhe. Wassira atakuwa katika mdahalo mkubwa utakaofanyika siku ya Jumapili kuanzia saa 9.00 Alasili mpaka saa 12. 00 jioni Ukumbi wa Blue Pearl, Mada itakayojadiliwa ni Katiba mpya na Hatma ya Bunge la Katiba, Washiriki wengine ni Tundu Lissu,Prof.Ibrahim Lipumba na Humphrey Polepole. . Wassira atawakilisha Chama na Serikali katika mdahalo huo. Don't miss on ITV live or in the Hall.

CHAMA CHAMA MAPINDUZI KINA WAJIBU WA KUISIMAMIA SERIKALI KUPITIA VIKAO HALALI .....HAPA NI MUDA MCHACHE KABLA NA WAKATI ...
18/07/2014

CHAMA CHAMA MAPINDUZI KINA WAJIBU WA KUISIMAMIA SERIKALI KUPITIA VIKAO HALALI .....HAPA NI MUDA MCHACHE KABLA NA WAKATI HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA BUNDA SHIME WANACHAMA WOTE TUENDELEZE UZALENDO UDUGU NA MSHIKAMANO WETU ILI TUYAFIKIE MAENDELEO ENDELEVU KWA TAIFA LETU.

SHUKRANI KWA WANANCHI WOTE WA JIMBO LA BUNDA KWA KUSHIRIKIANA NAMI KATIKA KUTEKELEZA AHADI NA ILANI YA CCM
18/07/2014

SHUKRANI KWA WANANCHI WOTE WA JIMBO LA BUNDA KWA KUSHIRIKIANA NAMI KATIKA KUTEKELEZA AHADI NA ILANI YA CCM

Address

Dar Es Salaam
123

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Yetu Kikwetu Kwetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tanzania Yetu Kikwetu Kwetu:

Share