05/10/2026
Heri ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kutoka KOM Group of Companies
Kwa KOM Group, wateja wetu ndio kiini cha kila tunachofanya.
Kwenda hatua ya ziada kwa mteja maana yake ni kusikiliza mahitaji yao, kuelewa wanachohitaji, kujibu kwa wakati, kutoa bidhaa na huduma bora, na kuendelea kutafuta njia bora zaidi za kuwahudumia.
Nyuma ya kila bidhaa bora kuna timu yenye kujituma. Kuanzia uzalishaji na udhibiti wa ubora, hadi mauzo, usafirishaji, huduma kwa wateja na vitengo vingine vya usaidizi ,kila mfanyakazi ana nafasi muhimu katika kuhakikisha wateja wetu wanapata bidhaa na huduma wanazoweza kuziamini.
Kwa wateja wetu, tunawashukuru kwa kuendelea kutuamini. Na kwa timu zetu, tunawashukuru kwa bidii, kujituma na kuhakikisha ubora unakuwa sehemu ya kila tunachofanya.