16/02/2026
𝐔𝐤𝐢𝐨𝐧𝐚 𝐔𝐧𝐚𝐩𝐞𝐰𝐚 𝐒𝐚𝐧𝐚, 𝐊𝐮𝐧𝐚 𝐊𝐢𝐭𝐮 𝐊𝐢𝐧𝐚𝐤𝐮𝐣𝐚… 𝐔𝐤𝐨 𝐓𝐚𝐲𝐚𝐫𝐢?
Kuna watu wanaomba wapate zaidi.
Lakini wachache wanaojiuliza — nitafanya nini nikipewa zaidi?
Ukiona Mungu anakupa sana, usifikiri ni bahati tu.
Ni ishara ya majukumu mapya yanayokuja.
Ni mtihani wa moyo wako.
Ni kipimo cha ukomavu wako.
Wengi wanapenda kupokea,
lakini si wengi wanaojiandaa kutoa.
Baraka zisipotiririka kwenda kwa wengine, zinageuka mzigo.
Neema isipotumika, inapoteza maana yake.
Kuna kiwango fulani ukifika,
hutakiwi tena kuhesabu ulichopewa —
unatakiwa kuhesabu uliowainua.
Watu wachache sana wanauelewa hili.
Na k**a wewe ni mmoja wao, basi ujue haukupewa kwa ajili yako tu…
umepewa kwa ajili ya wengine pia.
Usisubiri upoteze ndipo ujifunze kutoa.
Jifunze sasa. Hapo ndipo siri ya kuongezewa ilipo.
👉Usikose post k**a hii — bonyeza follow sasa hivi.