29/09/2021
ONYO! Hata Usifikirie Kujenga Nyumba Ya Makazi Mpaka Usome Kwanza Hii…
‘Hivi unajua kwamba ubora wa nyumba yako upo mikononi mwako? ’’
Je umekua ukifikiria kujenga nyumba ya ndoto zako lakini haufahamu nini cha kufanya ili kukamilisha ndoto hii? Ukweli ni huu hapa…
Mara nyingi wengi wetu tumekua tunajenga nyumba kwasababu tumeiona mahali fulani au kwa mtu na tukaipenda, yawezekana ikawa ni designing ya nyumba, ukubwa wa nyumba, finishing ya nyumba n.k . Ni sahihi kabisa kufanya hivi lakini yapo makosa makubwa yanayoweza kuku-cost hela nyingi ama kukufanya huko mbeleni kujutia na kutofurahia maamuzi ya kujenga nyumba yako (dream house)…
Ijumaa ya tarehe 11 June mwaka huu, wakati tupo ofisini tunaendelea na kujenga taifa na kujadili Mama jinsi anavoupiga mwingi, simu iliita. Kupokea ilisikika sauti ya mama mmoja mtumishi wa Mungu akisema angependa tufike site kwake Madale ana kazi yakutupatia, namba zetu alipewa na rafiki yake wa karibu, tukakubaliana tuonane kesho yake. Kesho yake tukafika mida ya mchana tukamkuta mwenyeji wetu ameshatutangulia lakini kitu cha kwanza tulichokigundua ni huyu mama hakuwa na furaha yaani ni wale watu ukimuangalia usoni unaanza kupanga maneno ya busara mapema kabisa. Kwa maelezo yake yeye alituambia ya kwamba awali baada ya kupata kiwanja na kupata michoro, alimtafuta fundi mmoja mwenyeji wa kule ambae anafahamika na amejenga nyumba nyingi akampa kazi ya ujenzi wa nyumba yake, baada ya ujenzi kumaliza hatua ya msingi ndipo mambo yakawa sio mambo tena….yule mama akaanza kuona nyumba yake ni finyu na sio k**a yalivyo matarijio yake na kilichomkatisha tamaa zaidi ni baada ya kutaka kufanya mabadiliko, fundi akaongeza dau zito huku kukiwa na mvutano wa hiki kinawezekana na hiki hapana…..hali hii ilimfanya mama huyu kukata tamaa na haswa akikumbuka hela ya kujengea nyumba ni mkopo aliochukua kutoka benki. Hela nyingine atatoa wapi tena?
Baada ya majadiliano ya kina na kuangalia michoro na kusikiliza mapendekezo ya yule mama, tulikuja kugundua ile michoro ni ilikua ameichukua kwa rafiki yake alietoka kumaliza ujenzi wa nyumba yake hivi karibuni.. Ili kuokoa gharama akaiomba na kumpatia fundi, naye fundi akasema mama kazi imeisha. Pigo kubwa lililokuja ni kwamba kutokana na maboresho aliyokua anataka kuyafanya, gharama yake ni kubwa mno hivo ikamlazimu yule mama kuagiza ujenzi usimame akusanye nguvu tubomoe ule msingi na kuanza ujenzi upya…..
Kabla hujanasa kwenye mtego huu, nitakupa siri 5 unapaswa kuzifahamu leo za mambo gani ya msingi na muhimu kuzingatia kabla hujaamua kujenga nyumba yako ;
1. Ijue familia yako ipoje : Aina ya nyumba unayotegemea kujenga ina uhusiano mkubwa na familia utakayoishi nayo kwani kila familia hutofautiana ukubwa, aina ya maisha na mahitaji ya kwenye nyumba husika. K**a wewe ni Bachela unategemea kuanzisha familia, au ni mume/mke mahitaji yako ya nyumba hayawezi kufanana na mzee mwenye wajukuu 5 aliestaafu na kupatiwa kiinua mgongo na akaamua kujenga nyumba. Mfano nyumba inajengwa ya ghorofa moja; chini vyumba vitatu na juu ina vyumba vine vyote self-contained, lakini nyumba hii ni ya mtumishi mstaafu mwenye familia ya watoto 3 na baada ya miaka yakufanya kazi kwenye malipo yake ya kiinua mgongo ametamani kujenga nyumba yakisasa ya makazi, watoto wake wote wanajitegemea. Ukiwa mtumishi mstaafu k**a mzee wetu huyu na unataka nyumba ya namna hii umejitengenezea mzigo mkubwa wa gharama….lakini kwa kijana ambae ni Bachela anayetarajia kuanzisha familia nyumba hii ni nzuri kwasababu itamsaidia katika kutunza na kulea familia yake.
2. Aina ya maisha yako yapoje : Kuna msemo unaosema usitumie zaidi ya unachokitengeneza, vivo hivyo katika ujenzi wa nyumba ni muhimu kuzingatia aina ya maisha (lifestyle) ya watakaoishi kwenye nyumba. Huwa inatokea muda mwingine mtu anaamua kujenga nyumba lakini katika hatua za mwishoni anakuja kugundua huu mjengo gharama zake za uendeshaji zipo juu sana ukilinganisha na kipato chake anaishia kuwa na msongozo wa mawazo na kukosa furaha. Ni vizuri na inashauriwa kabla ya kujenga nyumba yako uainishe ni mahitaji yapi ni ya lazima yawepo na yapi yanaweza kuwa optional kulingana na bajeti yako. Hii itakusaidia pia kuvipa vipaumbele vitu vya msingi zaidi kuwepo kwenye mjengo wako
3. Ukubwa wa Ardhi yako : ardhi au kiwanja ulichokinunua inabidi kiwiane na kile unachohitaji kukijenga. Kila kiwanja huwa kinakua na plot number pamoja na ukubwa husika wa kiwanja, hizi ni taarifa muhimu zinazomsaidia mchora ramani kutoa ramani ya kile unachokihitaji kwa kuzingatia ukubwa wa eneo husika. Haishauriwi kuiga mchoro ama kujenga nyumba uliyoiona kwa jirani kwa sababu mahitaji yako na yakwake yanatofautiana.
4. Wachora Ramani (Architects): Hawa ni wadau muhimu sana wakukamilisha kile unachokihitaji kutoka kwenye mawazo kwenda katika uhalisia. Hakikisha kila kinachowekwa kwenye ramani umeridhika nacho. Inashauriwa pia usiwe na haraka ama kuharakisha wachora ramani katika usanifu wa mjengo wako kwani michoro hii huakisi moja kwa moja kile mwenye nyumba anachotaka kiwepo kwenye nyumba yake kuanzia tofali hadi sehemu gani kopo la maua likae na liangalie upande upi….hivo ni vyema kuchukua muda wako vizuri katika kuhakiki na kujiridhisha katika michoro utakayotengenezewa na wachora ramani. Pro Tip : Usifanye mabadiliko site baada ya kuanza ujenzi, labda kwa mabadiliko madogo madogo lakini si mabadiliko yakurekebisha jengo (structural amendment). Ndio maana ni muhimu zaidi kurudia na kuhakiki michoro kabla ya kuanza ujenzi bila kujali ni muda gani unatumika kukamilisha mchakato huo.
5. Fundi Ujenzi vs Mhandisi: Ni ukweli usiopingika sekta ya ujenzi imekua kwa kasi mno kwa kipindi cha miongo miwili na hili kwa kiasi kikubwa kimechangiwa na mafundi ujenzi ambao wamekua mstari wa mbele na kichocheo kikubwa katika sekta ya ujenzi. Kosa kubwa linakuja pale ambapo mteja anatafuta unafuu wa bei na anakutana na fundi ambaye hana kazi. Nitakupa mfano kwa hili ili tuwe pamoja, Hebu vuta picha umenunua kiwanja chako maeneo ya Goba unataka kujenga nyumba ghorofa moja, baada ya kununua michoro unaongea na rafiki yako alietoka kumalizia mjengo wake maeneo ya Sinza anakuambia yeye anafundi wake mzuri wa ujenzi tena ni kiboko maana yeye alimpata kutoka site ya Kariakoo. Unachukua namba unampigia fundi sentensi ya kwanza kabisa anakuambia ‘ achana na wakandarasi wana bei sana, Mimi naweza kazi ya tofali, kupiga plasta, nondo pamoja na kupaua…’ tena anakuvuruga zaidi kwa kukuambia yeye kazi ni uhakika hana longo longo ila ukienda kwa mkandarasi utapigwa ‘cha juu’. Baada ya makubaliano na ujenzi kufanyika, haujakaa vizuri unashangaa sebule yako ya kibabe msimu wa mvua inageuka chemi chemi unaanza kusema majirani hawakupendi wanataka uhame… Unapaswa kufahamu ya kwamba ni kweli mafundi wengi wanaweza kufanya ujenzi wa nyumba yako lakini sio wote wanajua wanachokifanya. Hapa na maanisha sio mafundi wote wana ujuzi (technical skills) utakaowawezesha kufanya uchambuzi ni aina gani ya nyumba itafaa kujengwa kwa kuzingatia vitu k**a tabia ya udongo nyumba inapotaka kujengwa (nature of the soil) , topografia, uwezo wa udongo kuhimili jengo ( bearing capacity) n.k Asilimia kubwa ya mafundi huwa wanaamisha ujuzi aliopata kwa Mhandisi kutoka sehemu A na kupeleka ujuzi ule ule sehemu B, yaani vipimo na makisio ya kiutalaamu katika ujenzi wa nyumba iliopo Keko inachukuliwa inapelekwa k**a ilivyo kwenye kiwanja kilichopo Goba….kosa hili kubwa hupelekea mafundi wengi kufanya kitu kinachoitwa ‘ Over designing’ na madhara yake ni makubwa mno. Ni vyema zaidi ili uepuke gharama na usumbufu wa kufanya kazi mara mbili mbili kwenye mjengo wako, kamilisha ndoto zako za ujenzi kwa kuajiri Mhandisi yeyote aliesajiliwa na Bodi ya Wakandarasi kwa ngazi na ujuzi husika. Hii itakupa uhakika wa ujenzi wako kukamilika bila wasiwasi wowote kwani ujenzi wako utakua upo kwenye mikono salama ya watu wenye taaluma na weledi wakufanikisha ndoto yako iwe kweli….
Ni k**a bahati kwako, kwa sasa kuna njia rahisi ya kumaliza kabisa maswali, wasiwasi pamoja na kupata ushauri na ufafanuzi zaidi wa kina kuhusu dream house yako, tunatoa ushauri na madini k**a haya BURE kabisa bila gahrama ya tozo. Ili kupata huduma nyingi zaidi kutoka kwetu tupigie kupitia namba +255 714 819 888 au fika ofisi zetu zilizopo Jangwani / Ndovu Street, Dar Es Salaam Tanzania.