Elineemah Tech

Elineemah Tech Karibu sana mpenzi na mdau wa Teknolojia na sayansi ya Anga! Jukwaa lako la kupata update na info zo

01/04/2026

Yamebaki masaa masaa angalau manne (4) Safari ya kwenda Mwezini ianze!

25/03/2026

Hapa engineers wa NASA waliamua kuepusha kuchafua sayari ya Saturn
Safari ya mwisho ya chombo cha Anga Cassini Hyugens

27/02/2025

Hello ndugu zangu, hivi Mpo???😃
Ni siku nyingi sanaa😅😅

19/06/2024

Mpo?😊

NASA yapoteza mawasiliano na Helcopter robot yake (Ingenuity) huko mars baada ya mafanikio ya safari 71 za Helcopter hiy...
21/01/2024

NASA yapoteza mawasiliano na Helcopter robot yake (Ingenuity) huko mars baada ya mafanikio ya safari 71 za Helcopter hiyo hatimaye muda mfupi kabla haijatua ilipoteza mawasiliano na rover ya PERSEVERANCE. "Hatuna mawasiliano yoyote na ingenuity japo mainjinia wetu wanasogeza rover ya PERSEVERANCE karibu na ilipokusudiwa Helcopter robot hiyo kutua k**a tutapata kuiona kupitia camera za rover" wamesema hayo kupitia 'X' hapo awali "Twitter"

Ndege mpya iliyozinduliwa na NASA inayoitwa X-59 iliyotengenezwa na Kampuni ya Lockheed Martin imegharimu takribani dola...
15/01/2024

Ndege mpya iliyozinduliwa na NASA inayoitwa X-59 iliyotengenezwa na Kampuni ya Lockheed Martin imegharimu takribani dola za kimarekani Milioni mia mbili na hamsini (USD 250M), Lengo kuu sio kufikia spidi kubwa kwakua zipo ndege zenye speed kubwa kuliko hii.

X-59 inaweza kufikia spidi ya juu kufikia kilomita 1,510 kwa saa (1510km/h) sawa na mach 1.42,
Matoleo k**a F-35 zina spidi ya mpaka kilomita 1,900 kwa saa (1900km/h) sawa na mach 1.6 huku sauti ikiwa inasafiri kwa spidi ya kilomita 1,200 kwa saa (1200km/h)

Lengo kuu la X-59 ni kufanya utafiti wa kuweza kusafiri kwa spidi zaidi ya spidi ya sauti (Supersonic) bila kuzalisha sauti kubwa zaidi, sauti kubwa inayoitwa SONIC BOOM ina madhara kwa binadamu na viumbe wengine hivyo majaribio hayo yakifanikiwa tutaweza kuwa na ndege za abiria zenye spidi ya supersonic kwa marq nyingine tena!

Karibu sana Elineemah Tech kwa makala bora za sayansi na Teknolojia kwa Lugha ya kiswahili!

image: Lockheed Martin corporation
Source: Nasa
Publisher: Elineemah Mmari

14/01/2024

Enceladus!! Hii ni picha angavu zaidi (Ubora wa picha hii umepunguzwa na Facebook) ya mwezi wa sayari ya  Saturn, mwezi ...
19/11/2023

Enceladus!! Hii ni picha angavu zaidi (Ubora wa picha hii umepunguzwa na Facebook) ya mwezi wa sayari ya Saturn, mwezi huu pamoja na sifa zake nyingine moja ya sifa zake kuu ni mwezi wa barafu uso wake wote umeganda na kutengeneza barafu kutokana na Jotoridi dogo.

Mwezi huu una hali ya hewa ya ubaridi mkali mpaka kufikia Centigredi hasi Mia mbili na moja (-201°C) ambayo ni sawa na kipimo cha Fahrenheit hasi 330 (-330°F)

Picha hii inaonyesha uso wa mwezi huu ukiwa na mashimo (ambayo ni creta) na mipasuko mithili ya michirizi (ambayo ni mabonde na mito) Taarifa zilizokusanywa na chombo cha anga za mbali "Cassini spacecraft" wakati kilipopiga picha hii kikiwa umbali wa kilomita 61,300 mpaka kilomita 11,100 kutoka uso wa mwezi huu "Enceladus" Taarifa na data hizo zilibainisha kuwa chini ya uso huu wa barafu kuna bahari ambayo ndio hutoa chembe chembe kupitia nyufa za uso wa mwezi huu ambapo chembe chembe hizo zinapotoka angani kwenye hali ya ubaridi zaidi ndio huganda na kuwa vipande vya majabali ya barafu yanayounda ile pete ya sayari hiyo ya Saturn (🪐)

Bahari hiyo iliyo chini ya barafu hii ina miundo ya kemikali zinazoweza kuruhusu maisha ya viumbe hai.

Picha kwa idhini ya: NASA/JPL-Caltech/Space Science Institute.
Elineemah Tech
©Nov 2023.

Address

335665
Dar Es Salaam
12111

Telephone

+255654223036

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elineemah Tech posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Elineemah Tech:

Share