24/07/2024
First metals produced from Kabanga mineralization!
We have successfully produced the first-ever refined nickel, copper, and cobalt from our Kabanga Nickel Project through our parent company, Lifezone Metals (NYSE: LZM). This pilot-scale Hydromet Technology test work was conducted at Lifezone's Simulus Laboratory. This milestone comes nearly five decades after the deposit's initial discovery in 1975.
This accomplishment is a testament to the world-class potential of the Kabanga Nickel Project and sets a solid foundation for our future Kahama Refinery. It validates our commitment to establishing Tanzania as among key global sources of responsibly produced Class 1 nickel and other critical minerals.
We are proud to be at the forefront of realizing Tanzania's vision for full in-country value creation in the mining sector. The success of this pilot project brings us one step closer to full-scale production, with the Definitive Feasibility Study on track for completion in Q3 2024.
Tembo Nickel extends its gratitude to our dedicated team, government partners, and all stakeholders supporting this transformative project.
We look forward to the next phases of development as we work to unlock the full potential of Kabanga and Kahama for the benefit of Tanzania and the global green energy transition.
Metali za kwanza zimezalishwa kutoka kwenye madini ya Kabanga!
Tumefanikiwa kuzalisha nikeli, shaba, na kobalt zilizosafishwa kwa mara ya kwanza kutoka katika Mradi wetu wa Nikeli wa Kabanga kupitia kampuni yetu mama ya Lifezone Metals (NYSE: LZM). Kazi hii ya majaribio ilifanywa katika Maabara ya Simulus ya Lifezone. Mafanikio haya yanakuja karibu miongo mitano baada ya ugunduzi wa awali wa madini hayo mwaka 1975.
Mafanikio haya ni ushahidi wa uwezo wa kimataifa wa Mradi wa Kabanga Nickel na unaweka msingi imara kwa Kiwanda chetu cha baadaye cha Usafishaji Metali Anuai cha Kahama. Pia yanathibitisha dhamira yetu ya kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu vya kimataifa vya nikeli ya Daraja la kwanza na madini mengine ya kimkakati yanayozalishwa kwa uwajibikaji.
Tunajivunia kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza maono ya Tanzania ya uongezaji wa thamani ndani ya nchi katika sekta ya uchimbaji madini. Mafanikio ya majaribio haya yanatuleta hatua moja karibu na uzalishaji wa kiwango kikubwa, huku Utafiti Yakinifu ukiwa katika njia sahihi ya kukamilika ifikapo robo ya tatu ya 2024.
Tembo Nickel inatoa shukrani zake kwa timu yetu inayojituma, serikali ambayo ni mshirika wetu, na wadau wote wanaounga mkono mradi huu wa mageuzi.
Tunatazamia hatua zinazofuata za maendeleo tunapofanya kazi ya kufungua uwezo kamili wa Kabanga na Kahama kwa faida ya Tanzania na mpito wa nishati kuelekea nishati ya kijani duniani.
For full details, please follow this link: https://lnkd.in/epr_Mm5q