REJEA Hatimae

REJEA Hatimae Kuelimisha jamii juu ya kuiheshimu serikali na mungu wa mbinguni ili kilamtu aishi maisha ya kurejea kikamilifu kwa mungu

13/04/2020

HATARI YA KUAHIRISHA TOBA
Waebrania 3:15 hapo inenwapo, Leo, k**a mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, K**a wakati wa kukasirisha.

Jihadhari usiahirishe mambo. Usiahirishe kazi ya kuachana na dhambi zako, halafu tafuta kuwa na usafi wa moyo kwa njia ya Yesu. Hapo ndipo walipokosea maelfu kwa maelfu ya watu na kupata hasara ya milele.
Mimi hapa sitaongelea juu ya ufupi wa maisha na kutokuwa na hakika nayo; lakini ipo hatari ya kutisha - hatari isiyofahamika kwa namna itoshelezayo - katika kukawia kujitoa wakati inaposihi sauti ya Roho Mtakatifu wa Mungu, katika kuchagua kuendelea kuishi katika dhambi; kwa watu k**a hao kukawia huko ni jambo halisi.
Dhambi, haidhuru ifikiriwe kuwa ni kitu kidogo jinsi gani, inaweza kutendwa tu kwa hatari ya kupata hasara ya milele. Kitu ambacho tunakosa kukishinda, kitatushinda na kutuangamiza. Adamu na Hawa walijidanganya wenyewe kwamba kula matunda yaliyokatazwa si kosa kubwa linaloweza kuadhibiwa k**a Mungu alivyosema. Lakini katika jambo hilo dogo waliivunja sheria takatifu ya Mungu isiyobadilika kamwe, nayo ikamtenga mwanadamu mbali na Mungu, na kuifungulia milango ya mafuriko ya kifo na taabu zisizoneneka juu ya dunia yetu. Kizazi baada ya kizazi kilio cha daima cha maombolezo kimepanda juu kutoka katika dunia yetu, na viumbe vyote vinaugua na kuwa na utungu, k**a matokeo ya uasi wa mwanadamu. Mbingu yenyewe imeathirika kutokana na matokeo ya uasi wake dhidi ya Mungu. Kalwari yasimama k**a kumbukumbu ya kafara ya kushangaza mno iliyotakiwa kutolewa ili kufanya upatanisho kwa ajili ya uvunjaji wa sheria ya Mungu. Hebu na tusiifikirie dhambi kuwa ni kitu kidogo cha ovyo ovyo tu (Njia salama Uk 16). Yesu anakuita leo hii utubu na atakusamehe!! Unaweza ukaomba moyoni na anasikia,Omba sasa,tubu na atakusamehe!!
INGIA YOUTUBE ANDIKA MAHUBIRI TV ILI UPATE MASOMO MENGINE

03/03/2020

Address

Mwembechai
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when REJEA Hatimae posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category