18/10/2025
TAARIFA YA WANACHAMA WA FRIENDS OF MNARA SEC.
Sisi wanachama wa Friends of Mnara Secondary School tunayo heshima kubwa kuwasilisha rasmi taarifa hii kwa uongozi wa shule, Wanafunzi, Wahitimu, Mgeni rasmi na wageni waalikwa katika siku hii adhimu ya mahafali ya pili baada ya miaka 15 kupita.
Kupitia michango ya wanachama wetu, tumeweza kufanikisha upatikanaji wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya shule, ikiwemo:
Jezi pair 2
Mipira 3
King’amuzi cha Azam TV, pamoja na
Kifurushi cha mwezi mmoja (TZS 28,000/=) kwa ajili ya kulipia huduma ya Azam TV.
Vifaa hivi vimesafirishwa kutoka Dar Es Salaam na Anna Charles na vitakabidhiwa rasmi leo mbele ya hadhira ya mahafali k**a zawadi ya upendo, mshik**ano, na hamasa kutoka kwa wanachama wa Friends of Mnara Sec wanaoishi sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya nchi, kwa shule yetu ya Mnara Secondary School.
Tunatoa shukrani za dhati kwa kila mwanachama kwa moyo wa kujitolea, umoja na ari ya maendeleo iliyopelekea kufanikisha hatua hii muhimu. Huu ni mwanzo wa safari ndefu ya ushirikiano endelevu kati ya wanachama na shule yetu katika kuimarisha elimu, michezo na ustawi wa wanafunzi.
VIONGOZI WA FRIENDS OF MNARA SECONDARY SCHOOL
Mwenyekiti: Aid Olaf
Makamu Mwenyekiti: Faraja Mapengo
Katibu: Juma Hamisi Mohamed
Naibu Katibu: Habiba Malunda
Mweka Hazina: John Ndonde
Mhasibu Msaidizi: Anna Charles
WAJUMBE WA URATIBU WA KANDA
Ally Ngatame
Polika Sebastian
MRATIBU WA NIDHAMU NA USHIRIKISHWAJI au "baba la nidhamu": Aziz Kanjala
*SHUKRANI MAALUM*
Kwa heshima ya kipekee, wanachama wote wa Friends of Mnara Sec wanampongeza *Yusuf Mwijeje,* ambaye ingawa hajasoma Mnara Secondary School, lakini amekuwa nasi bega kwa bega katika kila hatua kupitia michango yake, hamasa na moyo wa upendo kwa maendeleo ya shule yetu.
LENGO NA DHIMA YA KIKUNDI
Friends of Mnara Sec kimejikita katika kujenga umoja na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya kijamii na kibinadamu, ikiwemo:
Kuchangia gharama za matibabu kwa mwanachama anapopatwa