18/10/2026
K**a tunataka kubadilisha industry yetu na kuipa tija, let us have no time for mediocrity.
Kufanya maandalizi ya quotation bila malipo ni aina ya unyonyaji wa kitaalamu, kwa sababu unatumia muda, resources na energy yako kutoa ushauri wa kitaalamu bure.
Sekta ya ufundi na ujenzi inahitaji kubadilika kutoka kwenye utamaduni wa kutoa makadirio ya gharama bila malipo kwenda kwenye mfumo wa kulipia tathmini za kitaalamu, hasa pale kazi inapohusisha ukaguzi wa eneo la kazi na uchambuzi wa kina.
Kwa nini? Kwa sababu ya hali k**a hii.
Umepima nyumba nzima ya mteja, umetathmini mahitaji yake, umeandaa quotation na umejibu maswali yake zaidi ya 100.
Mwisho wa siku, anakuambia amepata fundi mwingine anayefanya kazi hiyo kwa bei nafuu zaidi. Worse enough, anaweza kutumia quotation yako k**a reference kwa fundi mwingine.
Hapo ndipo unapogundua kuwa umetumia muda, ujuzi, uzoefu na rasilimali zako kutoa ushauri wa kitaalamu bila malipo.
Ukweli ni kwamba, kila mkandarasi au fundi anayefanya tathmini ya kina, kuandaa quotation na kutoa ushauri wa kitaalamu bila kutambua thamani ya huduma zake anachangia kudhoofisha sekta nzima.
Tunahitaji kubadilisha utamaduni huu.
Tujifunze kutofautisha kati ya makadirio ya awali ya gharama na tathmini kamili ya kitaalamu. Tuthamini muda wetu, ujuzi wetu na uzoefu wetu.
Kupata kazi kusiwe sababu ya kupuuza thamani ya utaalamu wetu. Tuna nafasi ya kuungana na kuweka utaratibu unaotambua thamani ya kazi yetu, ili wateja waelewe kuwa tathmini za kina na ushauri wa kitaalamu ni huduma zenye gharama.
K**a tunataka industry yenye tija, ushindani wa haki na huduma zenye ubora, lazima tuanze kwa kuthamini kazi yetu wenyewe.
Quotation inaweza kuwa bure, lakini utaalamu unaotumika kuiandaa una thamani.
Tuthamini taaluma yetu.