Stamigold Biharamulo Mine

Stamigold Biharamulo Mine STAMIGOLD Company Limited was incorporated on 28th October, 2013. The Company is a subsidiary of the State Mining Corporation (STAMICO)

INTRODUCTION
STAMIGOLD Company Limited was incorporated on 28th October, 2013. The Company is a subsidiary of the State Mining Corporation, engaging in prospecting, exploration, development, production and processing of gold, it also market gold within foreign markets. OPERATIONS
Following its incorporation as a government owned company, it currently own and operate STAMIGOLD Biharamulo Mine, the

gold mine in Biharamulo District formerly owned and managed by African Barrick Gold. The mine area comprises of two mineralized areas, the Eastern Zone ore body and the Western Zone and Mojamoja ore bodies; run of mine stockpile area, crushing plant, processing plant, fresh water reservoirs, waste water storage facilities and ancillary facilities. ACCESS
The mine site can be accessed by air using a private aerodrome registered as Muhama Aerodrome and by clay compacted roads joining the site with the Biharamulo and Kahama Highways. The site can be accessed by road from Kahama District centre as well as from Mwanza via Geita along the highway to Kigoma. CLIMATE
The annual average temperatures for the area range from 15 - 30°C. The total annual rainfall ranges between 800mm and 1100mm. The area is characterized by a bimodal type of climate whereby it has two rainy seasons (November to January) and (March to May). The annual evaporation rate is approximately 1100mm.

TAARIFA KWA UMMA
28/01/2019

TAARIFA KWA UMMA

STAMIGOLD YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KWA VITENDO DESEMBA 1,2018Kampuni ya Stamigold ambayo ni kampu...
07/12/2018

STAMIGOLD YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KWA VITENDO DESEMBA 1,2018

Kampuni ya Stamigold ambayo ni kampuni tanzu ya shirika la madini la Taifa STAMICO juzi (Desemba 1,2018) iliendeleza juhudi zake k**a taasisi ya serikali kupambana na maambukizi ya VVU kwa kuhamasisha upimaji na kutoa elimu kwa wafanyakazi wakandarasi na wananchi katika kata ya Kaniha. Zoezi la uhamasishaji na upimaji lilidumu kwa takribani wiki moja kabla ya kufikia kilele chake Desemba 1.

Stamigold kupitia idara ya maendeleo endelevu ikishirikiana na viongozi,matabibu na wauguzi wa vijiji (5) vilivyo ndani ya kata ya Kaniha, kuandaa zoezi la uhamasishaji wa upimaji wa hiari ili kuunga mkono juhudi za serikali kupitia wizara ya Afya katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI. Maadhimisho hayo yakibeba kauli mbiu ya mwaka huu isemayo PIMA, JITAMBUE, ISHI.
Ili kuwarahisishia wanachi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao, Stamigold iliandaa vituo (3) vilivyoendesha zoezi la upimaji ikiwemo kliniki ya Stamigold na zahanati za Mavota na Mkunkwa.
Aidha Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi Dkt. Venance B. Mwasse katika kuunga mkono juhudi za serikali ya tano ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli dhidi ya VVU/UKIMWI alijitokeza na kupima Afya yake mbele ya wanakijiji wa kijiji cha Mavota na hivyo kuongeza chachu kwa wanakijiji hao kujitokeza kwa wingi.

Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la upimaji kaimu meneja mkuu alipokea taarifa kutoka kwa Mganga msimamizi wa mgodi Dkt. Sarungi Mathias ikisema; katika zoezi hilo,wananchi kutoka kijiji cha Mavota waliyojitokeza ni 231 (wanaume 108 na wanawake 123), kijiji cha Mkunkwa wananchi 175 (wanaume 80 na wanawake 95), Stamigold 137 (wanaume 116 wanawake 21) hii inadhihirisha kuwa,wanawake wamehamasika zaidi ya wanaume na kuwataka waendelee kujitokeza kupima ili kujua Afya zao kwani VVU/UKIMWI haiui kinachoua ni magonjwa nyemelezi.

Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi Dkt Venance B. Mwasse alikuwa na haya ya kuzungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo; “Stamigold itaendelea kuunga mkono juhudi ya mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, ukizingatia mbunge wa wilaya yetu ya Biharamulo Mhe. Oscar Mukasa ndiye mwenyekiti wa k**ati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI tumefanya hivi kumuunga mkono kwa vitendo, na k**a kauli mbiu ya mwaka huu 2018 isemayo, PIMA, JITAMBUE, ISHI ikisisitiza watu kupima na kutambua Afya zao ili kuishi, VVU/UKIMWI hauui, kinachoua ni magonjwa nyemelezi, Ukipima na kutambua Afya yako utabadili mtindo wa maisha kulingana na majibu ya vipimo alisisitiza Meneja huyo.

Ikumbukwe: Stamigold tangu kuanzishwa kwake kwa shughuli za uchimbaji mwaka 2014 chini ya shirika la madini la Taifa STAMICO, imekuwa ikihamasisha upimaji kwa wafanyakazi na wakandarasi wa kampuni hiyo. Kwa mwaka huu kampuni imeongeza wigo kwa kushirikisha wanakijiji wa kata nzima ya Kaniha.

STAMIGOLD YANG’ARA MAONESHO YA KWANZA YA MADINI MKOANI GEITA 2018.Stamigold ni kampuni tanzu ya shirika la madini la Tai...
05/10/2018

STAMIGOLD YANG’ARA MAONESHO YA KWANZA YA MADINI MKOANI
GEITA 2018.

Stamigold ni kampuni tanzu ya shirika la madini la Taifa (STAMICO) inayomilikiwa na serikali ya Jamuhuri ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%) ikiwa ni kampuni ya pekee Kagera inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu iliyoshiriki katika maonesho ya kwanza ya teknolojia ya uchimbaji na uwekezaji wa madini ya dhahabu,Geita 2018.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Naibu Waziri Madini Mhe.Stanslaus Nyongo (Mb) tarehe 26 Septemba 2018 katika uwanja wa CCM Kalangalala akisisitiza migodi mikubwa na ya kati kuhakikisha inasaidia wachimbaji wadogo na jamii kwa ujumla ikiwa ni wajibu wa kisheria kuisaidia jamii kiuchumi na kijamii. Mhe. Stanslaus Nyongo alipata fursa ya kutembelea banda la Stamigold na alipokelewa na kaimu Meneja mkuu wa mgodi wa Stamigold Dr. Venance B. Mwasse na hivyo kupata maelezo ya namna mgodi wa serikali wa Stamigold unafanya shughuli zake kwa manufaa ya serikali na wananchi wote kwa ujumla.
Mgodi wa Stamigold Biharamulo ukiwa ni mgodi wa kati wa uchimbaji madini ya dhahabu wa pekee mkoani Kagera katika maonyesho hayo, uling’ara mara baada ya kupokea tuzo (Ngao) ya heshima k**a mshindi wa kwanza katika matumizi ya tekolojia ya uchimbaji madini dhidi ya migodi ya kati na midogo ukifuatiwa na Busolwa Gold mine tuzo hizo zilikabidhiwa na naibu waziri Madini Mhe. (Mb) Dotto Biteko mjini Geita 30, Septemba 2018.
Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akiwa mgeni rasmi katika kilele cha maonesho ya madini mjini Geita tarehe 30, Septemba 2018, alipata fursa ya kutembelea baadhi ya mabanda hasa ya wajimbaji wadogo na kujionea namna teknolojia ya uchimbaji na uchenjuaji dhahabu inakua nchini. Mhe. Kassim alikuwa na haya ya kusema; Tumeanza kuona mabadiliko makubwa katika sekta ya madini na kero nyingi za wachimbaji wadogo zimeanza kuondoka na ifikapo 2025 malengo ya serikali katika sekta ya madini yawe yamefikiwa,wakuu wa wilaya simamieni simamieni uanzishwaji wa vikundi vya wachimbaji wadogo na mabenki wekeni utaratibu wa kununua madini ya wachimbaji wadogo ili kuwasaidia. Waziri wa madini na wakuu wa mikoa endeleeni kusimamia makampuni ya madini kushiriki katika shughuli za kijamii, k**a sheria mpya ya madini inavyotaka.
Nae waziri wa Madini Mhe. Angela Kairuki alitumia fursa ya maonesho kuwaambia watanzania kuwa,wizara ya madini ina mpango ifikapo 2025 sekta ya madini ichangie pato la taifa kwa asilimia 10, hatua ya kuzuia kaboni (Carbon) nje ya mkoa inapopatikana imesaidia sana mkoa wa Geita pamoja na wachimbaji wadogo katika suala zima la utoroshwaji wa madini nchini. Pia viongozi wote wasimamie makampuni ya madini kutoa sehemu ya faida zao ikiwa ni uwajibikaji wa kampuni kwa jamii.
Aidha mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel mwenyeji wa maonesho hayo aliipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kubadilisha sheria ya madini hali iliyowezesha ushirikiano na makampuni ya madini kwa asilimia 100 katika kuimarisha huduma za jamii ikiwamo vituo vya Afya na sekta za elimu. Aliyasema hayo mbele ya mgeni rasmi Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).
Maonesho ya madini mjini Geita yalianza tarehe 24 Septemba na kufungwa 30 Septemba 2018. Muda wa Maonesho uliongezwa siku (3) hadi 3 Oktoba 2018 kwa ruhusa ya Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea ombi kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel. Maonesho hayo yakibeba ujumbe usemao TEKNOLOJIA BORA YA UZALISHAJI DHAHABU KWA MAENDELEO YA KIJAMII NA UCHUMI WA VIWANDA

KIKOSI CHA SBM FC KILICHOISAMBARATISHA GGM FC
31/07/2018

KIKOSI CHA SBM FC KILICHOISAMBARATISHA GGM FC

STAMIGOLD FC YAACHA SIMANZI KWA MASHABIKI  GGM FC GEITATimu ya soka ya kampuni ya Stamigold (SBM FC), siku za hivi (tar:...
31/07/2018

STAMIGOLD FC YAACHA SIMANZI KWA MASHABIKI GGM FC GEITA

Timu ya soka ya kampuni ya Stamigold (SBM FC), siku za hivi (tar:28/07/2018) imeacha simanzi kubwa kwa mashabiki, viongozi na wachezaji wa timu ya soka ya GGM Geita mara baada ya kuishushia kichapo cha bao moja kwa nunge katika mechi iliyoanza kutimua vumbi majira ya saa 10:30 jioni uwanja wa sekondari ya wasichana Nyankumbu Geita. Bao hilo lilipatikana kupitia mkwaju wa penati baada ya beki wa kati wa timu hiyo kuunawa mpira ndani ya eneo la 18 katika dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza,na bila ajizi nahodha msaidizi wa SBM FC Shekilango Mkwizu (KIMTI) aliukwamisha mpira nyavuni akimuacha golikipa wa GGM FC asijue la kufanya.

Bao lililodumu hadi timu hizo zinaenda mapumziko hali iliyowashangaza mashabiki na viongozi wa timu ya GGM ambayo inajitayarisha kushiriki ligi ya wafanyakazi wa mashirika,makampuni na taasisi za umma na binafsi (SHIMUTA) kitaifa,ligi hiyo inatarajiwa kutimua vumbi miezi michache ijayo mwaka huu.

GGM FC ilirudi uwanjani katika kipindi cha pili cha lala salama ikiwa na matumaini makubwa ya kusawazisha goli na ikiwezekana kuongeza mabao ya ziada ili kurudisha furaha za mashabiki wake waliyoonekana kukata tamaa. Katika kipindi cha pili GGM FC walianza kwa mashambulizi makali ya kustukiza hali iliyopelekea kumiliki mchezo kwa takribani dakika 29 bila mafanikio ya kupata bao la kusawazisha kwani walinzi wa timu ya SBM walionyesha umakini mkubwa hali iliyopelekea safu ya ushambuliaji ya GGM FC kushindwa kuleta madhara katika lango la SBM FC. Katika dakika za mwisho za kipindi cha pili SBM FC iliamka na kujibu mashambulizi dhidi ya mpinzani wake. Hadi filimbi ya mwisho ya mwamuzi SBM FC 1 GGM FC 0.

Aidha baada ya mchezo huo kocha wa timu ya GGM FC Bwana Ally Twist alikuwa na haya ya kusema; timu ya Stamigold imeonyesha kandada safi na ufundi wa hali ya juu hivyo wamestahiri kupata ushinda katika mchezo huu, lakini kupoteza kwa timu ya GGM FC imekuwa changamoto kwangu na viongozi wote,hivyo tutafanyia kazi udhaifu wa timu na kujiandaa vyema zaidi ili kusawazisha makosa tutakapokutana kwa mara nyingine.

Kwa upande wa Stamigold FC: Kocha msaidizi Godfrey Francis (Ag Com supervisor) alizungumza yafuatayo na mwandishi wetu; Nazipongeza timu zote mbili kwa kuonyesha kandada safi na la kuvutia, pamoja na ushindi huu SBM FC inatakiwa kujifua zaidi kwani mchezo wa marudiano utakuwa mgumu zaidi hivyo timu isijibweteke na ushindi huo bali kwa sasa tujikite kujitayarisha vyema na mchezo ulio mbele yetu.

Mkuu wa msafara wa timu ya SBM FC Muunda Nyakiroto (HR Officer), alitumia fursa ile kuushukuru uongozi wa GGM na viongozi wote wa timu ya GGM kwa mapokezi mazuri na ukarimu wao na kuahidi SBM kuendeleza uhusiano huo wa kimichezo uliyoanza na kuwataka kukubali mualiko wa kucheza mchezo mwingine wa kirafiki pale tutakapowahitaji.

STAMIGOLD FC YAMKARIBISHA VYEMA KAIMU MENEJA MKUU KWA USHINDI MNONO WA MABAO 3-0Kitengo cha Mahusiano ya jamii Mgodini k...
17/05/2018

STAMIGOLD FC YAMKARIBISHA VYEMA KAIMU MENEJA MKUU KWA USHINDI MNONO WA MABAO 3-0

Kitengo cha Mahusiano ya jamii Mgodini kikishirikiana vema na uongozi wa kijiji cha Mavota kiliandaa mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Stamigold FC dhidi ya Mavota FC siku ya jumapili (13 Mei,2018) ikiwa ni mahususi kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo, na pia kutumia fursa hiyo kumkaribisha Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi katika ushirikiano wa tasnia ya michezo kati ya Mgodi na vijiji vinavyouzunguka Mgodi,kwani ni mara yake ya kwanza kushuhudia timu ya Mgodi ikiingia uwanjani tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo mwishoni mwa 2017. Hata hivyo,Kaimu Meneja Mkuu akiongozana na baadhi ya viongozi wa SBM alikaribishwa kijijini hapo na uongozi wa kijiji Mavota ukiongozwa na Mwenyekiti wa kijiji Bwana Kulwa Malambo. Kabla ya kuanza kwa mchezo huo Meneja Mkuu Dr. Venance B. Mwasse akiwa mgeni rasmi katika mchezo huo wa kirafiki alisisitiza umoja,ushirikiano na mchezo wa kiungwana kwa pande zote mbili. Pia alitumia fursa hiyo kushukuru kwa ushirikiano waliyouonyesha na kuwataka vijana waonyeshe vipaji vyao kwa kucheza mchezo mzuri usio na vurugu wala uhasama.
Baada ya maelezo hayo ya Meneja mkuu kipenga cha mwamuzi kilipulizwa ikiashiria kuanza kwa mpambano huo, majira ya saa 10 na nusu jioni katika uwanja wa shule ya msingi Mavota,huku mashabiki wa kila upande wakijinasibu kushinda mchezo huo. Mchezo ulianza kwa kasi na kila upande ukiwa na hamu ya kupata goli la mapema na la kuongoza. Lakini hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Stamigold FC walikuwa wakiongoza kwa mabao mawili yaliyowekwa kimyani na mshambuliaji wao machachari Amani Emiry akipokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha Shekilango Mkwizu (Kimti) na kuukwamisha mpira nyavuni akimuacha Mlinda mlango wa Mavota FC asijua la kufanya.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wenyeji Mavota wakitafuta mabao ya kusawazisha wapinzani wao Stamigold wakitafuta bao la kuongeza ili kujihakikishia ushindi, hali iliyozaa matunda kwa SBM baada ya Hussein Mwinyimvua (Ball dancer) kupiga bao safi dakika za lala salama za kipindi cha pili,baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Ramadhani akitokea benchi. Bao hilo liliwanyong’onyesha na kupoteza matumaini ya ushindi kwa mwenyeji Mavota. Mpaka kipenga cha mwisho cha mwamuzi wa mchezo huo kinapulizwa kuashiria dakika 90 za mchezo zimemalizika Stamigold 3 wenyeji 0.
Mara baada ya mchezo huo mwandishi wetu alipata nafasi ya kuzungumza na kiongozi wa timu ya Mavota FC Bwana Lubinza nae alikuwa na haya ya kusema; Mchezo ulikuwa mzuri kwa pande zote mbili,Timu ya Mavota imecheza vizuri lakini wapinzani Stamigold walikuwa makini zaidi hasa katika safu ya ulinzi hali iliyopelekea washambuliaji wetu kushindwa kupenya ngome ya wapinzani wetu. Timu itajipanga na tunategemea katika mchezo mwingine tukikutana tena naamini tutaibuka na ushindi.
Aidha kocha msaidizi wa timu ya Stamigold Bwana Godfrey Francis ambaye pia ni kaimu Afisa Mahusiano ya jamii SBM aliwapongeza wachezaji wa pande zote mbili kwa kucheza mchezo wa kuvutia na kiungwana ukiongozwa na maamuzi ya haki kwa pande zote. Lakini pia alitumia fursa ile kuishukuru Menejimenti ya stamigold kwa ushirikiano waliyouonyesha hivyo kutia chachu na hamasa ya ushindi huo mnono. Pia alimaliza kwa kusema; Ushindi huu ni zawadi kwa Meneja Mkuu na menejimenti kwa ujumla kwani ameonyesha nia ya kuendeleza tasnia hii ya michezo Mgodini.
Hata hivyo Vijana wa Stamigold FC walionyesha kandanda safi lililopelekea watazamaji kufurahishwa na mchezo huo wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali ya kijiji,kata na mgeni rasmi Meneja Mkuu wa SBM Dr Venance B. Mwasse.

MATUKIO PICHANI

MENEJA MKUU SBM NA MGENI RASMI DR. VENANCE B. MWASSE (MWENYE TISHETI NYEUSI KATIKATI) AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WACHEZAJI WA TIMU YA MGODI WA STAMIGOLD MUDA MFUPI KABLA YA KUANZA MECHI V/S MAVOTA FC KATIKA UWANJA WA S/M MAVOTA.

07/03/2018

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amefanya ziara kwenye maeneo ya machimbo wilayani Nyang'hwale mkoani Geita.

Akiwa wilayani humo, Biteko alitembelea Mgodi wa Dhahabu wa Nyamigogo na eneo linaloombwa na Wachimbaji wadogo lililopo katika Kijiji cha Bululu.

Masuala aliyosisitiza Naibu Waziri ni;;;

*🔹Rais* anataka kuona Wachimbaji Wadogo wanakua na wanabadilisha maisha yao kupitia rasilimali zilizopo nchini ikiwemo madini.

*🔹Sheria ya Madini* iliyokuwa ikitumika awali kabla ya Marekebisho ya Mwaka 2017, haikumpa haki Mtanzania lakini hivi sasa Inatamka bayana kwamba rasilimali zote ikiwemo madini ni mali ya Watanzania

*🔹Maeneo ambayo hayaendelezwi* na hakuna taarifa yoyote, Leseni kwenye maeneo hayo zitafutwa.

*🔹Suala la CSR;* kila Mwekezaji anapaswa kuandaa mpango wake na kisha kuuwasilisha Halmashauri ili kupitishwa na kisha kuanza utekelezaji wake

*🔹Kutunza takwimu* za Uendeshaji wa mradi k**a Sheria inavyoelekeza katika kifungu cha 106 ambacho kinamtaka kila mwenye leseni kutunza kumbukumbu na kifungu kinachofuata kinampa mamlaka Afisa Madini kumpatia adhabu k**a itakua ameshindwa kutunza kumbukumbu husika

*🔹Local Content;* Sheria Mpya imeelekeza _minimum requirement_ za local content na Migodi inapaswa kujitathmini kuona imetekeleza kwa kiasi gani

*🔹Wajibu wa Mchimbaji Madini* ni kufuata Maelekezo, kuwa mwaminifu, Kulipa Kodi na kuacha kutorosha madini ili kujiletea maendeleo.

*🔹Jukumu la Serikali* ni kuwaondolea Watanzania changamoto mbalimbali zinazowakabili

*🔹Eneo la Bululu,* Wachimbaji wasifanye haraka. Wavute subira kwani leseni ya eneo hilo muda wake unamalizika Tar 30 Machi, 2018 ambapo Serikali itatatazama namna ya kuwapatia eneo waliopo kwenye vikundi.

*🔹Wachimbaji* wawasilishe orodha ya vikundi kwa Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Madini ili kuanza mpango na utaratibu wa ugawaji wa maeneo husika.

*🔹Leseni zote za Nyang'hawale* zitachambuliwa ili kubaini ambazo hazijaendelezwa kwa ajili ya kuvipatia vikundi vya wachimbaji wadogo.

*🔹Mwekezaji* anatakiwa kushirikiana na Jamii inayomzunguka ili kuboresha mahusiano na hivyo kuwa na tija kwenye shughuli zake.

*🔹Ugawaji wa maeneo* utazingatia vikundi na sio mtu mmoja mmoja ili iwe rahisi pia kupatiwa msaada na Serikali.

09/01/2018

*SERIKALI YAITAKA STAMIGOLD IJIENDESHE KIBIASHARA*

🔹Katibu Mkuu Madini atoa siku 14 kwa uongozi kuwasilisha mpango mkakati

Serikali imetoa siku 14 kwa kampuni ya Stamigold, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu uliopo Biharamulo mkoani Kagera, kuandaa mpango mkakati wa kibiashara, utakaobainisha namna itakavyojiendesha pasipo kuitegemea Serikali.

Agizo hilo lilitolewa jana, Januari 6, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alipotembelea Mgodi huo na kuzungumza na Menejimenti pamoja na wafanyakazi wake.

Profesa Msanjila alisema kuwa lengo la Serikali kupitia Wizara ya Madini ni kuona kampuni tanzu hiyo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), inajiendesha kibiashara na kiushindani ili ipate faida stahiki na kulinufaisha Taifa k**a ilivyo dhamira ya kuanzishwa kwake na siyo vinginevyo.

"Menejimenti ya Kampuni, Bodi pamoja Menejimenti ya STAMICO, nawapa hadi tarehe 21 mwezi huu, kila upande uwe umewasilisha mapendekezo ya kimkakati yanayobainisha namna gani Stamigold itaweza kusimama yenyewe na kujiendesha kiushindani k**a zilivyo kampuni nyingine za kibiashara. Kwa upande wetu, Kamishna wa Madini na mimi Katibu Mkuu pia tutakuja na mapendekezo yetu."

Akifafanua zaidi, Katibu Mkuu alisema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kampuni ya Stamigold hivyo haitakubali kuona mgodi huo unaendeshwa kwa hasara. "Kila mmoja awajibike kwenye eneo lake," alisisitiza.

Alisema, pamoja na kuwa Stamigold ni kampuni ya Serikali lakini imesajiliwa na Taasisi inayotoa leseni za biashara ya Brela, hivyo inapaswa kujiendesha k**a zilivyo kampuni nyingine za kibiashara.

"Kampuni ya Serikali ambayo haifanyi biashara haiendi kujiandikisha Brela. Ninyi mnafanya biashara hivyo lazima mfanye kazi kibiashara."

Aidha, Profesa Msanjila aliutaka uongozi wa kampuni kuhakikisha unaweka wazi taarifa zote za mapato na matumizi kwa wafanyakazi wote ili waelewe wanazalisha kiasi gani, wanapata faida kiasi gani, matumizi ni kiasi gani na k**a kuna hasara ibainishwe wazi.

Alifafanua kuwa utaratibu wa kuweka wazi mapato na matumizi kwa wafanyakazi wote utaondoa manung'uniko kwani mfumo wa kibiashara ni kumlipa mfanyakazi kulingana na mapato. "Huwezi kumlipa mtu mshahara hata pale ambapo hazalishi. Hii siyo sawa kibiashara maana lazima utapata hasara. Huu ndiyo ukweli ndugu zangu. Tubadilike. Hakuna hela ya kuchezea."

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, John Nayopa alimhakikishia Katibu Mkuu kuwa maagizo yote aliyoyatoa yatatekelezwa ndani ya wakati. Aidha, aliwataka wafanyakazi wa Stamigold kutoa ushirikiano kwa kutoa maoni na ushauri wao wakati wa kuandaa mpango mkakati huo utakaoiwezesha kampuni kujiendesha kibiashara.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu aliambatana na viongozi wengine wa Wizara akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimaliwatu, Miriam Mbaga, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahaya Samamba, Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Kagera, Paschal Bundala na Mhandisi Migodi kutoka wizarani, Kungulu Kasongi.

01/08/2017

SERIKALI, WADAU KUANDAA RIPOTI YA KWANZA YA KITAIFA YA UTEKELEZAJI WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza imeanza maandalizi ya ripoti ya utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu tangu Tanzania kuridhiria Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye ulemavu mwaka 2009.
Katika kufanikisha suala hili, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa kikao kazi kinachoshirikisha wadau wa haki za watu wenye ulemavu nchini ili kushirikiana katika maandalizi ya rasimu ya awali ya ripoti ambayo itajadiliwa,kuboreshwa na hatimaye kuwasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni hatua stahiki katika utekelezaji wa Mkataba wa Haki za watu wenye Ulemavu.
Kikao kazi hiki kinafanyika Mkoani Morogoro kuanzia leo tarehe 31 Julai 2017 mpaka tarehe 2 Agosti 2017 kwa lengo mahususi la kua na uelewa wa pamoja wa mfumo wa uandaaji ripoti za haki za watu wenye ulemavu wa Umoja wa Mataifa,kujadili na kutathmini utekelezaji wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu,kutoa elimu kwa wadau kuhusu usimamizi na ulinzi wa haki za watu wenye ulemavu na kuandaa rasimu ya awali ya haki za watu wenye ulemavu.
Akifungua kikao kazi hicho,Ndugu Erick Sh*tindi , Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Vijana,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu ameeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 35 sehemu ya i na ii, ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu, kila nchi inapaswa kuwasilisha ripoti ya kitaifa miaka miwili mara baada ya kuridhia mkataba husika jambo ambalo Tanzania haijwahi kulitekeleza kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya ripoti hiyo.
“Kwa mantiki hiyo,maandalizi ya ripoti hii yamekuja wakati muafaka na itaifanya Tanzania kuingia katika historia ya kutekeleza mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ikiwemo haki za watu wenye ulemavu na kwa ujumla nchi ilishaanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kutunga Sheria ya watu wenye ulemavu (The Persons with Disabilities Act,2010)”.anasistiza Katibu Mkuu Sh*tindi.
Naye Bi. Sarah Mwaipopo, Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Katiba na Haki za Binadamu,kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa Serikali inao wajibu kisheria kuratibu maandalizi ya ripoti na kutolea taarifa masuala mbalimbali ya utekelezaji wa haki za binadamu nchini k**a ilivyoainishwa katika kifungu cha 14 cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ( Section 14 of the Attorney General (Discharge of Duties) Act,2005).
Pamoja na Katiba, Sheria na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa kutambua haki za watu wenye ulemavu, Bwana Coomaaravel Pyaneandee, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Haki za watu wenye ulemavu ya Umoja wa Mataifa aneleza kuwa zipo changamoto ambazo zimeendelea kuwepokatika usimamizi na utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu ambazo ni pamoja na ukosefu wa takwimu sahihi za idadi ya watu wenye ulemavu,unyanyapaa katika jamii na ngazi ya familia,kukosekana mfumo mzuri wa elimu jumuishi,asasi za kiraia kushindwa kutumia nafasi yake kufanya kazi vizuri na serikali hivyo kushindwa kupaza sauti ipasavyo,kutokua na uelewa kuhusu watu wenye ulemavu na mahitaji yao na ukosefu wa miundombinu stahiki katika sehemu mbalimbali kwa watu wenye ulemavu.
Wadau wanaoshiriki katika maandalizi ya rasimu ya awali ya ripoti ya haki za watu wenye ulemavu ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Tanzania Bara na Zanzibar,Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania,Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania, Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Chama cha Walemavu wenye Utindio wa Ubongo,Chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi,Wizara ya Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo,Jeshi la Polisi Tanzania,Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,Wizara ya Afya Zanzibar,Chama cha Watu walioumia Uti wa mgongo Tanzania,Under the Same Sun,Wizara inayoshughulikia masuala ya uwezeshaji wazee,watoto na watu wenye ulemavu Zanzibar na Chama cha Wasioona Tanzania.

MASAA MILIONI MBILI YA MAFANIKIOTunarudi nyuma ya wakati na kukumbuka mwaka mmoja uliopita tulipoanza safari yetu ya usa...
05/07/2017

MASAA MILIONI MBILI YA MAFANIKIO
Tunarudi nyuma ya wakati na kukumbuka mwaka mmoja uliopita tulipoanza safari yetu ya usalama. Sio watu wengi nje ya timu yetu wanaelewa kwamba tunaweza kufanya shughuli zetu za uchimbaji kwa kuzingatia usalama na afya kwa kiwango cha hali ya juu. Lakini tulifanya, tumefanya, na wewe k**a mshirika wa Stamigold pia ulifanya kazi kwa usalama kwa nafasi yako!
Kufanya moja ya shughuli za hatari pasipo madhara na bila kutokea ajali inayoweza kusababisha kupoteza masaa ya kazi ni kitendo cha ujasiri halisi wenye weledi na pia kuleta tija na heshima kwa wote na kampuni kwa ujumla.
Tunajivunia mafanikio haya mazuri ya mwaka mmoja yaani siku 365 ikiwa ni zaidi ya masaa milioni mbili (2,000,000) ya kufanya shughuli zetu bila kusababisha ajali na kupoteza masaa ya kazi (LTI)
Mimi, wewe, sote ni mashujaa wa kweli wa usalama. Umefanya, tumefanya vizuri!
Hongera Sana!
Kwa kumaliza mwaka bila kupata majeraha na kupoteza masaa ya kazi.
Tumefanya Tumeweza Asante sana.

“Kazi yetu ya kwanza na jukumu letu kubwa ni usalama wako”

Ramadan Karim
01/06/2017

Ramadan Karim

15/05/2017

STAMIGOLD EXPECTS BUMPER HARVEST

THE government owned gold mining company Stamigold is set to undertake a record mining of 120,000 ounces of gold worth over 350bn/- in the next two years.
0 Comments
All is set for the job expected to start next month with the Company’s General Manager Mr Denis Sebugwao saying the explorations have already indicated the possibility of attaining the historical harvests.

According to Mr Sebugwao, the explorations undertaken in the Western Zone area of the mine site have shown the deposits amounting to 26,000 ounces and that of the Eastern zone of more than 85,000 ounces.

“We are glad to announce this historical milestone achieved by our public mining entity with the two areas showing great potential in gold deposits never achieved before and which will be the biggest since the mining commenced in 2014,” he said.

However, he said the discovery of gold in those areas will require heavy investment of nearly 44 million US dollars (around 90bn/-) with strategies already in place to secure the funds from different sources.

Giving a brief statistics, Mr Sebugwao said up to March this year, the company had managed to produce over 51,000 ounces and at least 5,000 ounces of different concentrates all worth 127bn/- Due to the recorded income, the company has paid different revenues to the government of around 35bn/- while Corporate and Social Responsibilities (CSR) obligations worth 515m/- have been offered in the villages surrounding the mine so far.

Mr Sebugwao maintained that a number of explorations will be undertaken in the future including the ongoing ones in T 7 area and nine other sites with prospects of attaining over 70,000 ounces that will help in increasing the life span of the mine for another two years.

Other master plans in the pipeline include the expansion of the processing plant so that it might increase the capacity to at least twice of the present with the investment expected to cost over 15 million US dollars.

“Reduction of production cost is one of the major targets and in achieving that we plan to purchase brand new mining machines worth 12 million dollars thanks to the Exim Bank of China which has agreed to sign a loan at an affordable interest rate of 2 percent payable in the period of five years,” he said. The purchase of own machines will ease the company from spending 10m/- a year for rented equipment from the private dealers.

Another achievement communicated by Mr Sebugwao was the agreement for the connection of power from the national grid that will be made possible before end of next year if all goes well, again relieving the company other millions of money currently paid for running power generators.

However, the DM pleaded for continuous support from the government so that the company can manage to effectively undertake its operations and commended the efforts by the Ministry of Energy and Minerals which is about to allocate 10bn/- for funding different costs for at least the next six month.

Address

Plot No. 417 UN Road
Dar Es Salam
P.O.BOX78508

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Stamigold Biharamulo Mine posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Stamigold Biharamulo Mine:

Share

Category