Walter Habari Tanzania.

Walter Habari Tanzania. TUPO KUKUHABARISHA. Karibu mpendwa upate habari na kuchangia mada mbalimbali.

Bweni la Wasichana Lateketea kwa Moto Kiteto, Mbunge Ole Lekaita Awatia Moyo Wanafunzi.Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Edward...
14/05/2026

Bweni la Wasichana Lateketea kwa Moto Kiteto, Mbunge Ole Lekaita Awatia Moyo Wanafunzi.

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Edward Ole Lekaita, amefika katika Shule ya Sekondari Engusero wilayani Kiteto kutoa pole kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza bweni la wasichana shuleni hapo.

Mbunge huyo ametembelea eneo la tukio na kujionea madhara yaliyosababishwa na moto huo kabla ya kupata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi pamoja na walimu kwa lengo la kuwapa faraja na kuwatia moyo baada ya kupatwa na janga hilo.

Akizungumza shuleni hapo, Wakili Ole Lekaita amesema jambo la muhimu zaidi ni kwamba hakuna madhara ya kibinadamu yaliyotokea licha ya moto huo kusababisha uharibifu wa bweni la wanafunzi.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda watoto wetu katika janga hili. Kitu cha msingi ni kwamba watoto wetu wote wako salama,” alisema.

Aidha amewataka wanafunzi kuendelea kuwa na moyo wa subira huku akiwasisitiza kuendelea na masomo yao bila kukata tamaa kutokana na tukio hilo.

Mbunge huyo pia amewataka wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kuwaombea wanafunzi hao ili waweze kuvuka kipindi hicho kigumu kwa utulivu na mshikamano.

Mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

TANZANIA YATOA SOMO KWA NCHI ZA SADC KUHUSU USIMAMIZI WA MAAFA.Tanzania imeendelea kung’ara katika ukanda wa Kusini mwa ...
13/05/2026

TANZANIA YATOA SOMO KWA NCHI ZA SADC KUHUSU USIMAMIZI WA MAAFA.

Tanzania imeendelea kung’ara katika ukanda wa Kusini mwa Afrika baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mifumo madhubuti ya usimamizi wa maafa, hatua inayozifanya nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujifunza kupitia uzoefu wake.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya wakati akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe. Balamagamba Kabudi wakati wa Mkutano wa Sita wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa nchi wanachama wa SADC unaofanyika mjini Masvingo, Zimbabwe.

Amesema Tanzania imefanikiwa kuimarisha mifumo ya kuzuia, kupunguza madhara, kujiandaa na kurejesha hali baada ya maafa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya uratibu wa maafa nchini.

Kwa mujibu wa Mhe. Mmuya amesema moja ya mafanikio makubwa ni kuanzishwa kwa Kituo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Majanga na Tahadhari ya Mapema (National Emergency Operation and Communication Center Situation Room), ambacho kinafanya kazi saa 24 kila siku kufuatilia na kuchambua taarifa za majanga.

“Kwa kupitia kituo hiki, Serikali imeweza kupata taarifa za mapema kuhusu majanga yanayoweza kutokea, kufanya uchambuzi wa madhara na kuweka mikakati ya haraka ya kukabiliana nayo,” alisema Mhe Mmuya

Aliongeza kuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za wakati halisi yamechangia kuongeza ufanisi wa maamuzi na kurahisisha utoaji wa taarifa rasmi kwa wananchi kuhusu namna ya kujiandaa dhidi ya maafa.

“Tunatumia takwimu za sasa na za zamani kutabiri hatari zinazoweza kujitokeza, jambo ambalo linaisaidia Serikali kupanga kwa usahihi hatua za kurejesha hali na kuendelea kulinda maisha ya wananchi,” alisisitiza.

Aidha, aliwaalika wajumbe kutoka nchi wanachama wa SADC kutembelea Tanzania ili kujionea namna mifumo hiyo inavyofanya kazi pamoja na ubunifu unaotumika katika usimamizi wa maafa.

Mkutano huo wa siku nne umezikutanisha nchi 16 wanachama wa SADC.

13/05/2026

Mkuu wa Wilaya Mbulu Ajinasibu Kufikika Kirahisi kwa Wananchi Bila “Password”

Michael Semindu amesema viongozi wanapaswa kuwa karibu na wananchi na kusikiliza changamoto zao kwa wakati ili kujenga imani na kuharakisha maendeleo ya jamii.

Semindu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Ufana wilayani Babati katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Wazazi kimkoa yaliyofanyika kata ya Ufana wilayani Babati.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo, Semindu alijinasibu kuwa yeye ni mmoja wa wakuu wa wilaya nchini anayefikika kirahisi bila “password”, akieleza kuwa mwananchi anahitaji kupiga simu moja tu na kupata huduma au mawasiliano yake moja kwa moja.

Amesema viongozi wanapaswa kuondoa urasimu usio wa lazima unaowafanya wananchi washindwe kufikisha matatizo yao kwa wakati, huku akisisitiza kuwa ofisi za serikali zinapaswa kuwa sehemu salama na rafiki kwa wananchi wote.

Aidha, amewataka wazazi na walezi kuendelea kusimamia maadili ya familia na malezi bora kwa watoto ili kujenga taifa lenye nidhamu, uzalendo na mshikamano.

Maadhimisho hayo ya Wiki ya Wazazi kimkoa yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti ya mkoa wa Manyara.

13/05/2026

TAARIFA YA POLISI KUHUSU JAMES TEMBA.

Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne akizungumza na waandishi wa Habari.

Muigizaji Sinema wa nchini Nigeria Alex Ekubo 41, amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kansa.Mmoja ...
13/05/2026

Muigizaji Sinema wa nchini Nigeria Alex Ekubo 41, amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kansa.

Mmoja wa wanafamilia amefunguka kwa kusema Alex alifariki siku ya jana tarehe 11 May huku tatizo kubwa lililopelekea kifo chake ikiwa ni maumivu makali ambayo chanzo chake ni ugonjwa wa Kansa.

13/05/2026

Wazazi Watakiwa Kukuza Maadili na Uzalendo Kwa Watoto.

Mbunge wa Viti Maalum Tanzania Bara kupitia Jumuiya ya Wazazi, Catherine Canute Joachim amewataka wazazi nchini kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema na uzalendo ili kujenga jamii yenye amani na mshikamano.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Wazazi kimkoa yaliyofanyika katika kata ya Ufana wilaya ya Babati Vijijini mkoani Manyara, Dkt. Catherine amesema uzalendo ni msingi muhimu wa kudumisha amani ya taifa.

“Wazazi tuna wajibu mkubwa wa kuwajenga watoto katika maadili mema na uzalendo, kwani uzalendo ndio unaoleta amani na kulinda mshikamano wa taifa letu,” alisema Dkt. Catherine.

Aidha, amewataka Watanzania kuendelea kuilinda amani iliyopo nchini kwa kushirikiana katika kujenga taifa lenye utulivu na maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara, Jannes Darabe amesema jumuiya hiyo itaendelea kusisitiza malezi bora kwa wazazi ili kuhakikisha watoto wanakuwa katika misingi ya nidhamu, heshima na uwajibikaji.

Maadhimisho hayo ya Wiki ya Wazazi yalifanyika chini ya kauli mbiu isemayo, “Malezi bora na uzalendo ni msingi wa taifa.”

NAIBU WAZIRI MMUYA AWASILI ZIMBABWE KUSHIRIKI MKUTANO WA SITA WA MASUALA YA MAAFA.Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maend...
13/05/2026

NAIBU WAZIRI MMUYA AWASILI ZIMBABWE KUSHIRIKI MKUTANO WA SITA WA MASUALA YA MAAFA.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya (Mb), amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Sita (6) wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi unaofanyika Masvingo, Zimbabwe kuanzia tarehe 11 haadi 14 Mei, 2026.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Mmuya amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Balozi Suzan S. Kaganda na kuipongeza Tanzania kushiriki katika mkutano huo unaolenga kujadili maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa programu za kikanda na masuala ya kimkakati katika utekelezaji wa afua mbalimbali katika Usimamizi wa maafa kwa nchi za SADC.

Masuala mengine yaliyoelezwa na Mheshimiwa Balozi Suzani ni pamoja na Tanzania kuendelea kuzitangaza fursa zilizopo ikiwemo sekta ya utalii, uchukuzi pamoja na kilimo huku akiahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Zimbabwe.

Sambamba na hayo, mkutano huo utahudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya Usimamizi wa Maafa kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo ni fursa kwa Tanzania kuendelea kujitangaza Kimataifa kwa kuwa na mifumo thabiti ya Usimamizi wa Maafa pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Menejimenti ya maafa.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki katika Mkutano huo wa siku Nne ambapo umekutanisha wadau wa masuala ya maafa kutoka nchi kumi na sita wakiwemo wataalamu kutoka katika ngazi za Kimataifa pamoja na Mashirika ya Umoja wa Kimataifa.

Dkt. Catherine Agawa Taulo za K**e Kuwainua Wasichana ManyaraMbunge wa Viti Maalum Tanzania Bara kupitia Jumuiya ya Waza...
13/05/2026

Dkt. Catherine Agawa Taulo za K**e Kuwainua Wasichana Manyara

Mbunge wa Viti Maalum Tanzania Bara kupitia Jumuiya ya Wazazi, Catherine Canute Joachim amegawa taulo za k**e na sabuni kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndeki, wilayani Babati mkoani Manyara, ikiwa ni sehemu ya kuwapa moyo wasichana kuendelea na masomo yao wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Wazazi kimkoa yaliyofanyika katika kata ya Ufana wilaya ya Babati Vijijini, Dkt. Catherine amesema hedhi si ugonjwa wala sababu ya kuwafanya wasichana wakose masomo au kuacha shule.

Amesema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 20 ya wasichana waliobalehe huacha shule kutokana na changamoto zinazohusiana na hedhi, hali inayochangia kuporomoka kwa ndoto zao za maisha.

“Tunataka kuwajengea wasichana wetu mazingira ya kujiamini. Hedhi sio ugonjwa, msiache shule kwa sababu hiyo. Someni kwa bidii ili mtimize ndoto zenu,” alisema Dkt. Catherine.

Aidha, amewataka wanafunzi kutumia vizuri fursa ya elimu waliyonayo kwa kuwa elimu ndiyo msingi wa mafanikio na maendeleo ya taifa.

Maadhimisho hayo ya Wiki ya Wazazi yalifanyika chini ya kauli mbiu isemayo, “Malezi bora na uzalendo ni msingi wa taifa.”

Katika hafla hiyo viongozi wa Jumuiya ya Wazazi pamoja na wananchi waliohudhuria wameeleza kuwa msaada huo utasaidia kuongeza uelewa kwa wanafunzi wa k**e na kupunguza utoro unaotokana na changamoto za hedhi shuleni.

**e

DKT Catherine Joachim Awasili Manyara Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi.Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho...
12/05/2026

DKT Catherine Joachim Awasili Manyara Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi.

Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Mkoa wa Manyara, Catherine Joachim amewasili mkoani humo na kupokelewa na wenyeji wake wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara, Jannes Darabe.

Maadhimisho hayo ya kilele yanafanyika katika Kata ya Ufana, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, yakihusisha viongozi wa chama, wazazi, walezi pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumza kuhusu maadhimisho hayo, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara, Christina Masagasi, amesema wiki ya wazazi imelenga kuimarisha malezi bora kwa watoto pamoja na kujenga uzalendo katika jamii.

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Malezi bora na uzalendo ni msingi wa taifa” ni ujumbe muhimu unaowataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao katika kulea watoto wenye maadili mema na kuipenda nchi yao.

12/05/2026

MTAA WA VIWANDA KUZALIWA MAPEA: Watenga Hekari 20, Ajira Maelfu Kutarajiwa

Wananchi wa Kijiji cha Mapea kata ya Magugu Wilaya ya Babati mkoani Manyara wanatarajia kushuhudia mageuzi makubwa ya kiuchumi baada ya kuanza kwa mipango ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo katika kitongoji cha Msimbazi.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi wa kijiji hicho, Diwani wa Kata ya Magugu, Stanley Charles amesema tayari hekari 20 zimetengwa katika eneo la Msimbazi kwa ajili ya kuanzisha mtaa wa viwanda, hatua ambayo inalenga kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wananchi.

Amesema ujio wa viwanda hivyo utasaidia vijana na wananchi wa eneo hilo kupata ajira pamoja na kuongeza shughuli za biashara kijijini hapo.

“Tunataka kuona Mapea inakuwa kitovu cha shughuli za kiuchumi. Viwanda hivi vitasaidia wananchi wetu kujiongezea kipato na kukuza maendeleo ya kijiji,” amesema Stanley.

Kwa upande wake, Meneja wa SIDO Mkoa wa Manyara, Abel Mapunda amesema tayari wanaendelea na mazungumzo na mdau anayetarajiwa kushirikiana katika uwekezaji huo.

Amesema moja ya makubaliano muhimu yaliyofikiwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Mapea ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi sambamba na maendeleo ya viwanda.

Aidha, wananchi wa Mapea wamekubali kwa pamoja kutoa eneo hilo la hekari 20 kwa ajili ya kuanzisha mtaa wa viwanda katika kitongoji cha Msimbazi.

Wananchi wa kijiji hicho wamepongeza hatua hiyo wakieleza kuwa italeta maendeleo makubwa, kuongeza fursa za ajira na kuifanya Mapea kuwa moja ya maeneo yenye ukuaji wa haraka kiuchumi katika Wilaya ya Babati.

12/05/2026

*SILLO YUPO ESWATINI KUIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA MABUNGE .*

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daniel Sillo ameendelea kuongoza ujumbe wa Tanzania unaowakilisha Bunge la Tanzania katika Mkutano wa Mabunge ya nchi za Afrika, Caribbean, Pacific pamoja na Umoja wa Ulaya unaoendelea nchini Eswatini.

Mkutano huo unawakutanisha wabunge na viongozi mbalimbali kujadili masuala ya maendeleo, ushirikiano wa kiuchumi, biashara, uwekezaji pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya.

Ujumbe wa Tanzania unashiriki katika majadiliano mbalimbali yenye lengo la kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, maendeleo ya vijana, usalama wa chakula pamoja na matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi.

Aidha, ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unaendelea kudhihirisha nafasi ya nchi katika kuimarisha diplomasia ya kibunge na ushirikiano wa kimataifa.

Address

Manyara

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Walter Habari Tanzania. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Walter Habari Tanzania.:

Share