24/11/2021
MMILIKI MGODI VS MWEKEZAJI (TAJIRI)
kuna mtu anamiliki mgodi (LEEENI YA PML) ila hela ya kuuendesha HANA, ila kuna TAJIRI anapesa zake ila mgodi HANA, hawa watu 2 wakishirikiana mnaweza nufaika na rasilimali madini.
wewe tajiri utaingia mkataba na wamiliki wa mgodi k**a wa miaka 7 wa kuendesha kazi za mgodi kwa pesa zako (100%) na mgodi ukianza uzalishaji wewe tajiri unachukua asilimia 60% ya MAPATO ya mgodi na wamiliki wa mgodi utawapa asilimia 40%.
mnaweza fanya hivi ila mnaweza fanya kwa namna ingine piA, kikubwa wewe tajiri unatakiwa kabla hujawekeza pesa zako kwenye huo mgodi na hujafunga mikataba na wamiliki wa mgodi kuhusu swala la asilimia unatakiwa kuwanza uangalie mambo ya msingi kwenye huo mgodi then ndio ufanye maamuzi ya wewe kuwekeza pesa zako au kutokuwekeza. na baazi ya mambo hayo ya wewe kuyatizama ni k**a vile.
1. historia ya mgodi, ni lazima k**a muwekezaji upate taarifa kamili za mgodi unaotaka kuwekeza historia yake k**a je ulishawahi toa madin??
2. GEOLOGY ya mgodi iko vipi, hapa ndio pakufanyia kazi sana upajue VIZURI maana ukishindwa kupata taarifa sahihi za hapa ndio unaona watu leo hiii wanakosea ku-invest kwenye uchimbaji wa madini mpaka mitaji inakata, geolojia ya eneo husika ndio ww itakufanya ujue uwekeze nguvu kiasi gani hadi kufikia hatua ya kuvuna madini, hapa ndio patakapo kusaidia ww kujuwa ni mtaji kiasi gani unahitajika kuwekeza ili kuendesha shuhuri za uchimbaji wa mgodi husika na kumbuka kila mgodi unakuwa na geolojia yake tofauti na mgodi mwingine, hapa tajiri unaetaka kuendesha mgodi unatakiwa upate taarifa zifuatazo:
A. madini katika mgodi husika yapo kwa wingi gani na yapo umbali gani? swali hili ni tata kidogo hususani k**a huna utalamu wa kijeolojia walau k**a una elimu ya jeolojia kidogo unaweza fanya tasmini roughly japo pia bila zana SAHIHI ni vigumu
B. vipi eneo hilo mwamba wake upoje, laini au mgumu hapa mwisho wa siku itatusaidia ww kujuwa utumie mashine gani kuchimba maana k**a ni mwamba laini basi unaweza tumia tindo, sururu chepe ila k**a ni mwamba mgumu hapa tajiri uanze kutafuta compresa , diga uchoronge hivyo uandae mpunga zaidi
C. vipi eneo lina maji sana , k**a lina maji tajiri unatakiwa ununue mamashine ya kunyonya maji mgodini maana mgodi ukiwa na maji hapo kazi zitafanyika kwa tabu hivyo ununue mapump ya kutosha hivyo utenge bajeti...
HIVYO HIZI TAARIFA ZA KIGEOLOJIA NDIO ZINAKUSAIDIA WW TAJIRI KUJUWA HUO MGODI UNAHITAJI KUWEKEZWA PESA KIASI GANI HADI KUFIKIA UZALISHAJI NA UKISHA TAMBUA HILI NDIO SASA UNAWEZA KUKAAA NA WENYE LESENI KUPANGWA SWALA LA ASILIMIA YAO NA YAKO, MAANA K**A UWEKEZAJI NI MKUBWA SANA UNATAKA KUFANYA MFANO UNATAKA KUWEKEZA BILIONI 2 KWENYE MIGODI WAO KATIKA UNUNUZI WA VIFAA NA MASHINE ZA KUCHIMBA ENEO HILO HAPO HAKIKISHA KUFANYA HAYA:
1. kwanza kwa pesa ndefu k**a hiyo funga nao mkataba wa muda mrefu hata miaka zaidi ya 10 maana usije wekeza bilioni 2 na ukaingia nao mkataba wa mwaka 1 na wenzako mkataba ukiisha ukiwaambia kuongeza mkataba wanagoma wakati ww umewekeza BILIONI ZAKO.
2. k**a unawekeza pesa nyingi k**a hivi au mfano wa hivi hakikisha wewe tajiri unawapa asilimia ndogo zaidi wenye mgodi sio tena 60% kwa 40% hii ni kwa uwekezaji wa kawaida. maana kila unapowekeza pesa nyingi zaidi risk ndio kwako inakuwa kubwa zaidi.
3. mkataba uweke wazi kuwa siku mkataba unapoisha na mkaamua msiendelee na mkataba mpya vipi mashine na mitambo iliyowekezwa kwenye huo mgodi nani abaki navyo?? tajiri ang'oe mitambo yake au mitambo ibaki katika MGODI hili swala liwe wazi kwenye mkataba wenu ili baadae lisije zua utata maana tajiri alikuta mgodi hauna kila kitu ila baada ya kuingia aliwekeza na kuweka miondombinu yote ya umeme, mashine na mitambo ya kisasa hadi eneo likaitwa mgodi leo anatoka vipi mitambo hiyo ibaki kuwa mali ya nani?? hili swala liwe wazi kwenye mkataba mlio sainiana
MAMBO NI MENGI SANA ,UNAKARIBISHWA KWA MASWALI