03/05/2024
: Lugha Yako, Kipaji Chako
Ipo Kasumba kwa Wazazi Kuaminishwa Kwamba Mtoto Kuzungumza Lugha za Kigeni k**a vile Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Kiarabu, nk ndiyo Uthibitisho wa Akili na Maendeleo sahihi ya kipaji chake.
Upotoshaji huu umepelekea Mtoto Kuhitimu Chuo Wakati Huo Hajiwezi na Amepoteza Uwezo Wake wa Asili wa akili, kufikiri na kipaji.
Matumizi ya Lugha za Kigeni Kujaribu Kuelemisha Vizazi ni Kuharibu Uwezo wa Watoto Kujitambua na Kupoteza Vipaji Asilia. Matumizi ya Lugha za Kigeni Yanadumaza Makuzi Sahihi ya Ubongo hususan pale Lugha Mpya [lugha Isiyotumika Mazingira Yanayomzunguka Mtoto] Inapotambulishwa katika Umri kati ya Miaka 10 mpaka 16. Katika Kipindi hiki sehemu inayopokea lugha mpya inakuwa imekomaa hivyo mtoto kutoimudu lugha na kutomudu kufikiri kupitia hiyo lugha.
Michezo ni Elimu, Burudani, Ajira, Afya, Taaluma, Maadili (Malezi), Tamaduni, n.k.
Kutambua na Kulea Kipaji cha mtoto ni Muhimu kwa Ustawi wa Maadili yetu, Kukuza Kiwanda cha Michezo na ajira, na Kutengeneza Umma Unaoelimika, Kuthamini Desturi ya Asili Yetu na kukuza uchumi wa taifa.
Chanzo: Mchapishaji wetu
Kukuza Vipaji na Kukomesha Kasumba kwenye Jamii
( Mwalimu Bora Daima efforts to identify and develop talents, and eradicate conscious and subconscious misconceptions https://www.facebook.com/mwalimu.bora.daima | .bora.daima; https://www.instagram.com/mwalimu.bora.daima | .bora.daima)