HEALTH PLANET

HEALTH PLANET Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from HEALTH PLANET, Biotechnology company, Mwanza.

Tunatoa huduma zifuatazo;
�Ushauri kuhusu matatizo ya mzunguko wa hedhi, ujauzito na ugumba.
�Ushauri kuhusu dalili za magonjwa mbalimbali ya wanawake, watoto na wanaume. Gharama ya Elimu fupi au ushauri kwa njia ya whattsap au facebook chats ni Tshs 2000 tu, lipa kwa MPESA no 0752354147, AIRTEL money 0784082190, halafu uliza swali lako kwa kubonyeza kwenye kitufe kilichoandikwa "Message'' hapo kwenye page, au tuma ujumbe Whattsap kupitia no 0752354147

BAKA JEUSI KWENYE NGOZI NA HATARI YA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI.Baka Jeusi kwenye ngozi hufahamika kitaalam k**a  , hut...
13/12/2022

BAKA JEUSI KWENYE NGOZI NA HATARI YA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI.

Baka Jeusi kwenye ngozi hufahamika kitaalam k**a , hutokea kwenye ngozi hasa sehemu za nyuma ya , na , hali hii huambatana na kuwashwa ngozi, kujikuna na hatimae kuvimba sehemu hizo, waathirika wa tatizo hili hupaka dawa za fangasi mara kwa mara bila kupona.

Hali hii hutokea hasa kwa watu na wenye uzito kupita kiasi(over weight), inaweza kujitokeza mara kwa mara katika ukoo.

na homoni ya Insulin kuwa sugu na kushindwa kufanya kazi yake. Kumbuka homoni ya insulin hufanya kazi ya kupunguza sukari ya ziada kwenye damu.

cha homoni ya insulin kushindwa kufanya kazi ndo huusika pia na kusababisha ugonjwa wa Kisukari aina ya pili yaani Type 2 Diabetes Mellitus.

hii pia hutokea kwa wanawake wenye ugonjwa wa vimbe nyingi kwenye mayai yaani Polycystic Ovarian Syndrome ambao pia hupata mabadiriko katika mzunguko wa hedhi, kushindwa kushika ujauzito, kukosa hamu ya tendo la ndoa, ngozi kuota nywele nyingi zaidi, ndevu, na sauti kuwa nzito k**a ya mwanaume.

vingine ni pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa k**a Niacin, Prednisolone, na vidonge vya kupanga uzazi, baadhi ya saratani k**a sarata ya damu(lymphoma) na utumbo mpana pia husababisha hali hii.

Tembelea HEALTH PLANET kwa mada kemkem za Afya na Ushauri kwa gharama nafuu zaidi.

JE UNAFAHAMU BAADHI YA STYLE ZA   HUSABABISHA UGONJWA WA KUNYONYOKA NA KUPOTEZA NYWELE?                 wa kunyonyoka na...
21/10/2022

JE UNAFAHAMU BAADHI YA STYLE ZA HUSABABISHA UGONJWA WA KUNYONYOKA NA KUPOTEZA NYWELE?


wa kunyonyoka na kupoteza nywele hufahamika kitaalam k**a Alopecia
jinsia zote japo hutokea zaidi katika umri wa utu uzima kwa wanaume.
kutokea kwa mda au ukawa kudumu.
wa nywele kwa kiwango kikubwa husababisha .

HUSABABISHWA NA NINI?
1. Hali ya kurithi katika ukoo, husababisha kupoteza nywele kwa kiwango kikibwa hasa katika umri wa utu uzima kwa wanaume.

2. Mapungufu katika vichocheo(hormones) k**a androgens na vile vitokanavyo na tezi ya thyroid.

3. Baadhi ya dawa za kutibu
a)saratani,
b)shinikizo la damu,
c)magonjwa ya magoti k**a arthiritis na gout,

4.Msongo wa mawazo na mshtuko wa kihisia(emotional stress).

5.Kusuka na ku set nywele kwa kupitiliza pia husababisha nywele kunyonyoka kwa sababu ya kuvutika sana( style hizi hasa (mkia wa nguruwe), (mistari ya mahindi))

05/10/2022

MWANAMKE ALIEKAA MDA MREFU BILA KUPATA UJAUZITO,

ZIFAHAMU DALILI NA ALAMA AMBAZO HUSAIDIA WATALAM WA AFYA KUJUA CHANZO CHA TATIZO.

Takwimu zinaonesha asilimia 15.5 ya wanawake hushindwa kupata ujauzito, wakati walio katika hali ya kawaida hupata ujauzito ndani ya mwaka 1 wa majaribio.

Pia asilimia 6.7 ya wanawake walioolewa, walio katika umri wa kuzaa(miaka 15 hadi 44), hushindwa kubeba ujauzito ndani ya mwaka 1 wa ndoa.

Dalili au alama zifuatazo husaidia wataalam wa Afya kujua chanzo cha tatizo kwa mwanamke alieshindwa kubeba ujauzito kwa mda mrefu.

💥Mabadiriko katika mzunguko wa hedhi

💥Kunenepa sana na Unene kupita kiasi, uwiano wa uzito na urefu (BMI) unaozidi 25.

💥Kuwa na ndevu au nywele nyingi kwenye ngozi k**a mwanaume.

💥Kuwa na sauti nzito k**a mwanaume

💥Kukosa hamu ya tendo la ndoa

💥Matiti kuvimba, kuuma na kutoa maziwa

💥Kuwa na baka jeusi kwenye ngozi hasa sehem za siri, mapajani, shingoni, nk
- Ambalo sio la kuzaliwa nalo na halijatokana na ajali.

💥Maumivu ya kichwa ya mda mrefu

💥Matatizo ya kuona

Tembelea Helath Planet kupitia Facebook au whattsap kupitia nambal, 0752354147
Ushauri wa Afya kwa gharama nafuu sana

UNAFAHAMU NINI KUHUSU UGONJWA WA UPELE  KWENYE NGOZI,    ni ugonjwa wa upele na muwasho kwenye ngozi, unaosababishwa na ...
12/09/2022

UNAFAHAMU NINI KUHUSU UGONJWA WA UPELE KWENYE NGOZI,

ni ugonjwa wa upele na muwasho kwenye ngozi, unaosababishwa na wadudu wadogo wanaofanana na chawa wanaofahamika kitaalam k**a Sacrcoptes Scabei au Mite.

ya watu Milioni 300 wanaathirika na ugonjwa huu duniani kote, huathiri watu wa rika lolote, hasa watoto, na watu wazima wasiofanya usafi binafsi.

na kuenea kutoka mtu hadi mtu kwenye jamii k**a familia, shule n.k kwa njia ya kugusana ngozi na kuchangia nguo au mashuka.

kuu ni vipele(k**a inavyoonekana kwenye picha), vinavyotokea sehemu yoyote kwenye ngozi, hasa kwenye mikunjo ya ngozi, huambatana na kuwashwa na kujikuna, na kusambaa kutoka mtoto mmoja hadi mwingine.

huusisha matumizi ya dawa ya kuua wadudu wanaosababisha ugonjwa huu kwa kutumia dawa ya kupaka kwenye ngozi.

binafsi, kuoga, kufua nguo, kupiga pasi, kuepuka kugusana ngozi na mtu/mtoto mwenye ugonjwa husaidia kudhibiti ueneaji kutoka mtu hadi mwingine.

ya familia nzima ya mtoto mwenye upele, na kudhibiti ueneaji wa ugonjwa shuleni ni muhimu sana.

na hivyo magonjwa ya ngozi yanayosababisha upele na muwasho ni mengi, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya allergy(mzio) na fangasi, inashauriwa kumuona mtaalam wa afya kwa ajili ya matibabu ili kupata tiba stahiki na kuepuka matumizi ya dawa kiholela.

na , .

 , NINI CHANZO.Tatizo la kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu linasumbua watu wengi kwenye jamii.Health Planet tun...
22/08/2022

, NINI CHANZO.

Tatizo la kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu linasumbua watu wengi kwenye jamii.
Health Planet tunakuandikia Sababu kubwa 4 zinazopelekea mtu kupata hali hiyo;

1. Ugonjwa wa maambukizi ya Amiba, minyoo ya tumbo na kichocho kwenye njia ya chakula,

2. Ugonjwa wa Bawasili, ambao hutokea endapo mishipa midogo ya damu kwenye njia ya haja kubwa hujaa damu na kuvimba (hali hii huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia, maumivu ukiwa umekaa, na kuhisi kitu k**a kidole kwenye njia ya haja kubwa)

3. Kuchanika kwenye njia ya haja kubwa, hutokea kwa sababu ya kujisaidia choo kigumu ambacho huchana na kusabisha damu kutoka ikiwa imechanganyika kwenye haja kubwa.

4. Saratani ya Utumbo mpana pia inahusika na kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu

Je unapata tatizo hili, HEALTH PLANET tunakupa ushauri na elimu zaidi kuhusu tatizo ulilonalo.

Karibu tuandikie kwenye page yetu kwenye kitufe kilichoandikwa 'Message'

MATUMIZI YA    NA HATARI YA KUSABABISHA UGONJWA WA AKILI    na kwamba matumizi ya bhangi huuzawadia mwili hali ya kujisk...
23/05/2022

MATUMIZI YA NA HATARI YA KUSABABISHA UGONJWA WA AKILI

na kwamba matumizi ya bhangi huuzawadia mwili hali ya kujiskia furaha sana, kemikali ya Tetrahydrocanabinol(THC) kwenye bhangi hupunguza uwezo wa kufikiri na kupunguza umakini wakati wa kufanya shughuri mbalimbali, huathiri sehemu ya ubongo inayoitwa Cerebelum na Basal ganglia kitendo ambacho husababisha kukosa balance, kushindwa kuratibu matendo(coordinate) na kuathiri hali ya kukaa au kusimama wima(maintaining posture)

💥Hii ndio sababu ya watumiaji madereva kushindwa ku control vyombo vya moto na kusababisha ajali barabarani💥

ya bhangi yanaweza kusababisha ukichaa kwa mda mfupi(Acute psychosis) na kusababisha mtumiaji kuona au kuskia vitu visivyokuwepo(hallucinations) na kuhisi au kuamini vitu visivyokuwepo(delusions), tabia zisizo za kawaida k**a kuvua nguo, kula na kuvaa uchafu majalalani(bizzare behaviours) nk

💥Hali hii ndio husababisha watu wanaotumia bhangi kutenda makosa ya kisheria na kuishia magerezani k**a vaadhi ya waathirika walioko kwenye gereza hosputali za wagonjwa wa akili💥

Karibu HEALTH PLANET kwa ajili ya ushauri na elimu kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya.

JE UNAFAHAMU KUNYONYESHA KUNAWEZA KUTUMIKA K**A NJIA YA UZAZI WA MPANGO?👉Katika hali ya kawaida mama anaenyonyesha mwili...
07/04/2022

JE UNAFAHAMU KUNYONYESHA KUNAWEZA KUTUMIKA K**A NJIA YA UZAZI WA MPANGO?

👉Katika hali ya kawaida mama anaenyonyesha mwili wake hutengeneza homoni aina ya Prolactin inayosaidia kutengeneza maziwa.

👉Homoni hii pia huzuia ovari za mwanamke kupevusha mbegu za k**e, katika hali hiyo kuzuia mwanamke kubeba ujauzito wakati ananyonyesha.

👉Kutumia kunyonyesha k**a njia ya uzazi wa mpango hufahamika kitalam k**a Lactational Amenorrhea Method(LAM), mama anaenyonyesha anaweza kutumia njia hii kuzuia kupata ujauzito mapema.

👉Ni njia salama ya uzazi wa mpango kwa sababu ni ya asili, haina athari kwenye homoni za kijinsia na inakubalika kulingana na kanuni za madhehebu mbalimbali.

👉Inaweza kuzuia ujauzito kwa zaidi ya asilimia 98.

👉 Kupanga uzazi kwa njia ya kunyonyesha inawezekana k**a;
💥Mama hajaanza kuona siku za hedhi,
💥Mama ananyonyesha kila mara mtoto anapohitaji kunyonya kila siku angalau kila baada ya masaa 4 mchana na usiku,
💥Mtoto hajazidi umri wa miezi 6.

👉Mama anaelisha mtoto kwa kukamua maziwa hawezi kufanikiwa kutumia njia hii, mfumo wa kuzuia kupata ujauzito unakuwepo tu k**a mama ananyonyesha mtoto.

Je unahitaji kupata elimu au ushauri wa kiafya? Tembelea page yetu au tufikie kupitia no 0752354147

INAWEZEKANAJE MWANAMKE KUBEBA UJAUZITO WAKATI AKIWA MJAMZITO.Katika hali ya kawaida mwanamke akishatunga ujauzito,👉Homon...
22/03/2022

INAWEZEKANAJE MWANAMKE KUBEBA UJAUZITO WAKATI AKIWA MJAMZITO.

Katika hali ya kawaida mwanamke akishatunga ujauzito,
👉Homoni aina ya progestrone huongezeka ili kukuza ujauzito uliotungwa na kuzuia mayai(mbegu) nyingine za k**e kupevuka.
👉Pia uteute mzito hutengenezwa na kuziba kwenye mlango wa kizazi ili kuzuia mbegu za kiume kupita.

hali inayotokea kwa nadra sana, inayofahamika kitaalam k**a ,
👉 Homoni ya progestrone na uteute huwa havitengenezwi kwa kiwango cha kutosha.
👉Katika mzunguko wa hedhi wa mwezi unaofuata hali hii hufanya ovari za mwanamke kutengeneza na kupevusha mbegu nyingine ya k**e wakati mwanamke huyo ni mjamzito tayari.
👉Pia uhaba wa uteute mzito kwenye mlango wa kizazi huruhusu mbegu za kiume kupita na kurutubisha mbegu ya k**e iliyopevuka.

💥Hali hii husababisha kutunga ujauzito mwingine na mtoto mwingine kukua kwenye mji wa mimba.
💥Watoto wawili hukua wakitofautiana umri kwa tofauti ya wiki 2 hadi 4.
💥Ikitokea ujauzito wa kwanza na wa pili ulitungwa kwa mbegu za wanaume wawili tofauti, watoto wanaokua tumboni huwa wa baba tofauti.

Madhara yake ni nini?
👉Mtoto mkubwa anapokomaa, uchungu huanza na watoto wote hulazimika kuzaliwa kwa wakati mmoja
👉Hali hii haifahamiki sana hata kwa wataalam wa afya walio wengi, kinachoonekana ni kwamba mama hujifungua mapacha watoto wawili ambao mmoja ametimia na mwingine ni njiti(hajatimia miezi 9)
👉Wataalam wa afya wanaojua hali hii na hasa k**a imegundulika mapema wanaweza kupunguza madhara ya kuzaa mtoto njiti kwa kusubiri mtoto mdogo akue zaidi na kuzaliwa katika umri atakaokua bila matatizo mengi.

tunakusogezea mada za afya za kipekee naxkukupa ushauri kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya, Karibu namba yetu 0752354147 kwa ajili ya ushauri .

NAMNA YA KUTUMIA   KUPANGA UZAZI NA KUEPUKA KUPATA MIMBA ZISIZOTARAJIWA.  wa mpango ni muhimu kwa wale wanaotaka kufanik...
21/03/2022

NAMNA YA KUTUMIA KUPANGA UZAZI NA KUEPUKA KUPATA MIMBA ZISIZOTARAJIWA.

wa mpango ni muhimu kwa wale wanaotaka kufanikisha malengo yao kabla ya kuamua kupata ujauzito na kuzaa mtoto/watoto. Pia ni muhimu kwa wenza au yule anaetaka kuzaa watoto wenye afya njema kwa kuweka nafasi ya kutosha kati ya mtoto na mkubwa wake, humpa nafasi mwanamke kurejea katika hali ya kawaida kiafya baada ya uzazi na kupata mda wa kufanya majukumu mengine.

ya kupanga uzazi kwa kutumia Kalenda, ni njia ya asili bora na salama inayoweza kumkinga binti au mwanamke asipate ujauzito katika kipindi ambacho haitaji,
👉Haina athari kwenye mfumo wa homoni za mwanamke au njia ya uzazi k**a zilivyo njia zingine za homoni au kitanzi.
👉Wenza au mtumiaji huitaji kutambua na kukwepa siku zenye uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito(Siku za hatari).
👉Ni njia inayohitaji ushirikiano kati ya wenza ili kukubaliana na kuepuka kufanya tendo wakati wa siku za hatari.

kutumia njia hii kwa usahihi ni muhimu mwanamke awe na
👉Mzunguko wa hedhi unaoeleweka, unaoweza kuhesabika mwanzo na mwisho wake.
👉Awe na mzunguko wa hedhi ulio kati ya siku 21, 28,hadi 35.
👉Awe na uelewa angalau wa kujua kusoma namba.
👉Awe na Kalenda ya ukutani au kwenye simu.

wanaochukua mda mrefu sana kuona siku zao, wasioingia au wanaoingia hedhi kwa kuruka mwezi/miezi au kuona matone kidogo sana ya damu kwa masaa machache ni vigumu kufanikiwa kutumia njia hii.

vya msingi kujua kabla ya kuanza kutumia kalenda
👉Mzunguko wa hedhi ni kipindi ambacho mbegu ya k**e hutengenezwa kwenye ovari na hupevuka pia maandalizi ya kupokea ujauzito hufanyika ndani ya mfuko wa uzazi na kuharibiwa k**a ujauzito haukutungwa.
👉Kipindi cha kwanza cha mzunguko ni wakati ambao mbegu ya k**e hutengenezwa kwenye ovari na kukomaa-huchukua takribani muda wa wiki 2(siku 14)
👉Kipindi cha pili cha mzunguko ni wakati ambao mbegu iliyokomaa hurutubishwa na mbegu ya kiume na muunganiko wake kusafiri hadi kwenye mji wa mimba ili kutunga ujauzito, 💥Pia ni kipindi ambacho k**a mbegu haikurutubishwa huandaliwa pamoja na ukuta wa ziada kwenye mji wa mimba( ulioandaliwa kupokea ujauzito) hutolewa nje ya mwili k**a damu kipindi cha hedhi. Kipindi hiki huchukua siku 14(kwa wenye mzunguko wa siku 28), siku 7(kwa wenye mzunguko wa siku 21(siku 21 kwa wenye mzunguko wa siku 35)
👉Siku za hedhi-ni siku ambazo mwanamke hutoka damu, kwa kawaida huchukua kati ya siku 3 hadi 7, Idadi ya siku za hedhi haina athari kwenye kuhesabu kufikia siku za hatari.
👉Siku ya mbegu ya k**e kupevuka na - ni siku ambayo mbegu ya k**e iliyokomaa hutoka kwenye ovari, ndio mda ambao k**a mbegu ya k**e itakutana na ya kiume hurutubishwa na kutunga ujauzito, ni kipindi muhimu ambacho wasiopenda kupata ujauzito huitaji kujua ili wakwepe kufanya tendo kwenye siku chache kabla, ndani ya siku yenyewe na siku chache baada. Kipindi hiki huitwa siku za hatari kwa wasiopenda kupata ujauzito.
💥Siku ya 14 ndio ambayo mbegu ya k**e hupevuka, kwa sababu ya uwezekano wa kuwahi kupevuka siku chache kabla au kuchelewa siku chache baada ya siku ya 14 kipindi cha siku za hatari huongezwa kutoka siku chache kabla ya siku ya 14 hadi siku chache baada ya siku ya 14. Kwa sababu hiyo siku za hatari huanzia siku ya 12 hadi ya 16 ya mzunguko, kwa sababu za kuongeza uwezekano zaidi wa kukwepa ujauzito siku za hatari zinaweza kuongezwa zaidi kuanzia siku ya 10 au 11 hadi ya 18 au 19.
💥Kipindi hiki pia huambatana na viashiria vingine k**a joto la mwili kuongezeka kidogo, kuwa na uteute mzito kwenye uke, kuongezeka kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

$Ili kutumia kalenda kupanga uzazi, Mwanamke anapoona damu za hedhi siku ya kwanza
👉Weka alama kwenye kalenda ya mwezi, mfano kwenye mchoro wetu siku za hedhi, period au bleed ni tar 23 hadi 26, hapa tarehe 23 ni siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi.
👉Hesabu kwa kufuata kalenda kuanzia siku ya kwanza ambayo ni tar 23, k**a mwezi utaisha endelea tu kwenye mwezi mwingine.
👉Weka alama X kuanzia siku ya 12 hadi ya 16 ya mzunguko, Hizi ndo siku ambazo wenza watatakiwa kujua ili waepuke kufanya tendo la ndoa au kutumia vizuizi k**a kondom na kukwepa kupata ujauzito.

tunatoa huduma ya kupitia mzunguko wa hedhi na kufundisha namna ya kujua siku za hatari kwa mtu mmoja mmoja kwa kuzingatia siku alizoingia kipindi cha hedhi na kalenda ya mwezi husika.
Ili kupata huduma hii karibu inbox whattsap no yetu 0752354147.

💥LEO TUANGAZE KUHUSU💥UMRI SAHIHI KWA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO, MADHARA YA MIMBA ZA UTOTONI NA MIMBA BAADA YA UMRI SAHIHI...
29/01/2022

💥LEO TUANGAZE KUHUSU💥

UMRI SAHIHI KWA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO, MADHARA YA MIMBA ZA UTOTONI NA MIMBA BAADA YA UMRI SAHIHI!!!
Karibu!!

👉Tamaa ya kutaka kufanikiwa maishani imeenea duniani kote. Hali imebadilika sana, jinsia ya k**e inataka kujitosheleza kwa kila kitu. Lakini mabadiliko ya kibaiolojia yanabaki vile vile mfano kuzeeka nk.

👉Mafanikio wanayowaza wengi ni utajiri wa pesa na elimu kubwa. Hii imesababisha wanawake wengi kusoma sana na kufanya kazi kupita kiasi, hata kupuuzia suala la kuzaa mapema.

👉Wengi wanashtuka ikiwa umri wao ni zaidi ya miaka 30, ndio wanakuwa na tamaa ya kuzaa. Kuchelewa kwao kuzaa kunaweza kuwa kwa taabu ama kuzaa watoto wenye matatizo mengi ya kiafya.

👉Kwa miaka mingi, wataalamu wengi wa afya ya uzazi bado wanaamini miaka 20-35 ndio umri sahihi kushika mimba na kuzaa.

👉Pia, wengi wakifikiri matatizo mengi ya uzazi huongezeka baada ya miaka 35 na huwa zaidi baada ya miaka 40.

👉Kwa wenzi wawili wanaoishi pamoja, kuchelewa kuzaa huathiri pia wenza wa kiume, ambapo mbegu za uzazi za mwanaume hudhorota kila mwaka upitao na watoto wamaotokana na wanaume wazee huwa na hatari zaidi ya kupata matatizo ya akili na matatizo ya chembe za urithi.

KUBALEHE

👉Kubalehe ni hatua muhimu sana lupotia ili kuweza kuzaa. Wastani wa kubalehe na kuvunja ungo kwa wasichana ni miaka 9-12 kwa sasa, ingawa miaka ya zamani ilikuwa kuanzia miaka 12-14.

👉Baada ya kubalehe binti anakuwa na uwezo wa kushika mimba, japokuwa uwezekano huongezeka zaidi kati ya miaka 20-30, baada ya hapa uwezekano huanza kupungua.

👉Kulingana na The American College of Obstricians & Gynecologists uwezo wa wanawake kuzaa hupungua katika umri wa miaka 32 na hupungua kwa kasi zaidi katika umri wa miaka 37.

👉Uwezo wa wanawake kuzaa hupungua vile umri unaongezeka kwa kuwa wanawake wanapobalehe wanakuwa na idadi kamili ya mayai katika ovari zao. Namba hii hupungua vile mwanamke anavyozeeka. Pia mayai hayazalishwi kiurahisi kwa wanawake wenye umri mkubwa ukilinganisha na mabinti wadogo.

👉Kulingana na National Institute for Health & Clinical Excellence (NICE) ya Umoja wa madola (UK), kwa wanawake wenye miaka 35, ni wanawake 94 kati ya 100 wanaweza kupata ujauzito wakifanya ngono kwa ukawaida ndani ya miaka 38, ni wanawake 77 kati ya 100 wanaweza kushika ujauzito.

👉Magonjwa ya njia za uzazi k**a Endometriosis na Uterine fibroids yanawatokea zaidi wanawake wenye umri mkubwa ambayo husababisha mwanamke kutoshika mimba.

👉Wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35 wanaoamua kushika ujauzito wanakabili hatari ya kupanda kwa shinikizo la damu. Kupanda kwa shinikizo la damu wakati wa ujauzito huathiri kondo la nyuma (Placenta) ambalo hutoa lishe kwa kijusi (kitoto kilicho tumboni) hali ambayo huathiri moja kwa moja ukuaji wake.

👉Pia, hatari ya kupata kisukari kwa wanawake wanaoshika ujauzito wakiwa na miaka 35 na zaidi, huongezeka sana. Kisukari kipindi cha ujauzito huongeza hatari ya kutoka mimba (Miscarriage), kuzaa mtoto mwenye kasoro au kuzaa mtoto mkubwa kupita kiasi.

TAFITI YA HIVI KARIBUNI

👉Jambo la kushtusha, ni matokeo ya utafiti uliofanyika Sweden, watafiti wanadai hatari ya matatizo ya uzazi huanza mapema tu pale mwanamke anapofikisha miaka 30.

👉Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la magonjwa ya uzazi (Journal of Obstetrics & Gynacology) uliofanywa na watafiti kutoka Taasisi ya Karolinska ya nchini Sweden umegundua katika nchi tajiri duniani wanawake huzaa wakiwa na umri mkubwa kitu kinachopelekea kuongezeka kwa hatari ya kuzaa watoto njiti (Preterm birth), ukuaji hafifu wa vichanga na kuzaa watoto wafu (Stillbirth).

👉Ili kubainisha hatari kati ya makundi tofauti ya umri ya wanawake wanaozaa kwa mara ya kwanza, watafiti walitumia takwimu za vizazi toka hospitali za Sweden na Norway, zilizokusanya taarifa za karibu wanawake milioni moja, kati ya mwaka 1990 na 2010.

👉Hatari ya kuzaa watoto njiti (Premature birth) na kuzaa watoto wafu huongezeka kuanzia miaka ya 30 ingawa toka zamani, miaka 35 ndio ilitambulika kuwa mwanzo wa hatari kwa wanawake kupata watoto, lakini utafiti huu mpya unataja mwanzo tu wa miaka 30 hatari ya kupata matatizo katika uzazi huanza.

👉Kwa kulinganisha kati ya kundi la umri wa miaka 25-29 na 30-34, wanawake wa miaka 30-34 wenye mimba za kwanza walikuwa na hatari ya kuzaa watoto njiti kwenye wiki 22-31 za ujauzito au kuzaa watoto wafu.

👉Kikosi cha watafiti kiligundua pia sababu zingine zinazoweza kuleta matatizo ya uzazi mfano wa sababu hizo ni k**a kuvuta sigara au kuwa mnene kuliko kawaida.

👉Ulla Waldenstrom, profesa wa kitengo cha afya ya wanawake na watoto katika taasisi ya Karolinska alisema : 'Tumeshangazwa na kuongezeka kwa hatari za uzazi katika umri mdogo sana.'

👉Prof. Waldenstrom aliendelea ; 'Wanawake wanaweza ona hatari ni ndogo ila kwa jamii kiujumla kuna idadi kubwa ya matatizo yasiyo ya lazima kwao wanawake wanaozaa baada tu ya miaka 30. Hivyo nashauri wanawake na wanaume wapewe taarifa mashuleni juu ya umuhimu wa umri katika uzazi.'

👉Alipoombwa ushauri kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 30 wanaotaraji kuzaa, Prof. Waldenstrom alisema ; 'Ushauri bora ni kuepuka uvutaji wa tumbaku/sigara na kuepuka unene, k**a inawezekana.''

KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI (MENOPAUSE)

👉Wataalamu wa afya wanasema kwamba mwanamke amekoma hedhi anapokosa kupata hedhi kwa miezi 12 mfululizo. Ni wanawake wachache hukoma kupata hedhi ghafula, yaani, wanakosa hedhi mwezi mmoja unakuwa mwisho wa kuipata.

👉Wanawake wengi huanza kipindi hiki wakiwa na umri wa miaka 40 na kitu, lakini kwa wengine huanza wakiwa wamechelewa wakiwa na miaka 60 na kitu.

👉Kutokana na mabadiliko ya kiwango cha homoni kinachotokezwa, huenda mwanamke akakosa kupata hedhi pindi kwa pindi, akapata hedhi wakati ambao hakutarajia au akavuja damu nyingi isivyo kawaida wakati wa hedhi. Pia huenda mwanamke akashuka moyo, hisia zake zikabadilikabadilika na hilo linaweza kumfanya alielie bila sababu, na pia asiwe makini sana na asahau mambo.

👉Kipindi cha kukoma hedhi huwa tofauti kwa kila mwanamke. Dalili zinaweza kuonekana kipindi hicho ni pamoja na joto la ghafula mwilini, ambalo huenda likafuatiwa na kuhisi baridi. Dalili hizo zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na kuishiwa na nguvu.

👉Baadhi ya wanawake hupatwa na joto la ghafla mwilini kwa mwaka mmoja au miaka miwili wakati wa kipindi hicho cha kukoma hedhi.

👉Wengine hupatwa na hali hiyo kwa miaka mingi na wachache sana husema kwamba wao hupatwa na joto la ghafula mara kwa mara maisha yao yote.

👉Ni busara mtu afanyiwe uchunguzi wa kiafya kabla ya kuamua kwamba joto la ghafula linasababishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa kuwa kuna matatizo mengine ya kiafya yanaweza kuleta joto la ghafula mfano ugonjwa wa dudumio, malaria, homa ya matumbo n.k

JINSI YA KUISHI VIZURI KIPINDI HICHO

👉Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kupunguza baadhi ya matatizo hayo mfano kuacha kuvuta sigara, kupunguza au hata kuacha kunywa vileo, vinywaji vyenye kafeini na vyakula vyenye sukari au vikolezo ambavyo vinaweza kusababisha joto la ghafula mwilini.

👉Kufanya mazoezi husaidia sana kupunguza matatizo yanayohusianishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kupunguza kukosa usongizi na kusaidia kuboresha hali ya kihisia na pia huimarisha mifipa na afya ya mtu kwa ujumla.

👉Ili kumsaidia mwanamke kukabiliana vizuri na kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi, huenda madaktari wakampa homoni, vitamini na madini, na dawa za kutibu kushuka moyo.

👉Pia ni jambo la busara kuwaambia uwapendao hali unayokabili ili wakuonyeshe upendo na wakupe msaada unaouhitaji wakati wa hali yako.

👉Kipindi hicho kinapokwisha, wanawake ambao hutunza afya yao, wanapata tena nguvu na kuendelea kufurahia maisha.

Asanteni sana kwa kufuatana nami, Karibu HEALTH PLANET

 KIPIMO KINACHOSAIDIA KUJUA SIKU ZA KUSHIKA UJAUZITO.💥Mwanamke hushika ujauzito kipindi anapokuwa amepevusha mbegu ya k*...
24/01/2022



KIPIMO KINACHOSAIDIA KUJUA SIKU ZA KUSHIKA UJAUZITO.

💥Mwanamke hushika ujauzito kipindi anapokuwa amepevusha mbegu ya k**e, Upevushaji wa mbegu ya k**e yaani ovulation hutokea katika siku za katikati za mzunguko wa hedhi, kati ya siku ya 12 hadi 16 kwa wanawake walio wengi ambao huwa na mzunguko wa siku 28.

💥Wakati wa kipindi cha upevushaji joto la mwili,uteute mzito kwenye via vya uzazi, na hamu ya tendo la ndoa huongezeka. Wanawake walio wengi hushindwa kubaini mabadiriko haya na kupita kwenye kipindi hiki bila kujua.

💥Pamoja na hivyo mzunguko wa hedhi unaweza kuwa tofauti kati ya mwanamke mmoja na mwingine, unaweza kuwa na idadi ya siku tofauti kati mwezi mmoja na mwingine au upevushaji kutokea siku tofauti tofauti kati ya mizunguko kila mwezi.

💥Hali hii husababisha mwanamke anaetaka kupata ujauzito kushindwa kujua au kupatia kipindi sahihi cha mbegu ya k**e inapopevuka ili ajiandae kushika ujauzito.

👉Kipimo cha kubaini kipindi cha kushika ujauzito hufahamika kitaalam k**a Ovulation test kit au Ovulation Predictor kit(OPK), Hupatikana kwenye maduka makubwa ya dawa(pharmacy)

👉👉👉Hupima uwepo wa homoni ya LH ambayo huongezeka mwilini masaa 12 hadi 36 kabla ya kupevusha mbegu ya k**e.

👉👉👉Kipimo cha strip(utepe) hufanana na kipimo cha ujauzito, hupimwa kwa kutumia sampuli ya mkojo, majibu husomwa kwa kuangalia mistari inayochora kwenye utepe baada ya kuuchovya kwenye mkojo.

👉👉👉Kina uwezo asilimia 97 wa kuonesha majibu sahihi. Majibu chanya huashiria aliepimwa atapevusha mbegu ya k**e baada ya masaa 12 hadi 36.

👉👉👉Mtumiaji huitaji kuanza kupima siku chache kabla ya kufika katikati ya mzunguko wake, kwa mzunguko wa kawaida wa siku 28, huanzia siku ya 10.

💥Baada ya kusoma majibu chanya, mtumiaji atahitaji kushiriki tendo la ndoa kuanzia siku aliyopata majibu chanya na kuendelea angalau kwa siku 3 ili kuongeza uwezekano wa kushika ujauzito.

💥Kipimo hiki hakisaidii kwa wanawake wenye mzunguko wa hedhi uliovurugika ambao hauna mpangilio sahihi wa kuelewa mwanzo kati na mwisho, hakisaidii kwa wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya yanayosababisha mwanamke kushindwa kushika ujauzito.

💥💥Kwa ushauri zaidi, Karibu

Address

Mwanza

Telephone

+255752354147

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HEALTH PLANET posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to HEALTH PLANET:

Share