28/12/2019
"Unaweza kurithi mali za baba yako lakini siyo thamani au hadhi yake. K**a baba ni Profesa utarithi vingi kwake lakini siyo Uprofesa wake, utafanya kazi ya ziada kuifikia hiyo hadhi.
imeandikwa (Luk. 6:40)
'Mwanafunzi hawezi kuwa mjuzi kuliko mwalimu wake, ila akihitimu, anaweza kuwa bingwa k**a mwalimu wake.'
Unaweza kupita njia nzuri ikakufikisha mahali pazuri lakini mahali hapo pasiwe mahali sahihi kwaajili yako. Unaweza kuwa na marafiki wazuri lakini si marafiki sahihi kwaajili ya maono yako. Usijione bora kuliko wenzako au huna thamani kuliko wenzako. Kuna mwanzo wa kila jambo na kuna mwisho wa kila jambo, hakuna majira yadumuyo. Hilo nalo litapita k**a mengine yalivyopita."