17/01/2024
MOYO WA MASIKINI 💔
Sehemu ya nne🌹🌹
Simulizi zetu page
Njombe Tanzania🌹
AYUNI ANAMCHUKUA KIBA NA KWENDA NAE MJINI
Kiba alionekana mshamba sana hakuna sehemu aliyo lala macho nje ya gari muda wote ,
WANAINGIA MJINI
Kiba aliachia meno yote nje kwa mshangao " kuzuri mjini " alisema Kiba kwa sauti kubwa AYUNI alimjibu tu kwa kifupi
" kuzuri ukiwa na pesa ukipaparikia mji ni mbaya sana huu ,magorofa haya hayana msaada wowote kwako, kuna makundi ya kila aina kuna marafiki wa kila aina ,ogopa watu wa mjii huu kuliko simba na chatu mnaoishi nao kijijini , kwa sababu adui ni vizuri ukamjua kuliko akawa rafiki yako ,siku atakayo kuzuru na uaminifu wako huijui , na pia binadamu anauwezo wa kuuwa simba na chatu ,na maanisha binadamu ndio hatari kuliko simba na chatu ,na maliza kwa kusema karibu mjini KIBASU"
Kiba alikaa kimya baada ya maneno mazito ya rafiki yake , walitembea umbali kidogoo foleni ikawa kubwa Kiba akaomba msaada afunguliwe mlango mkojo umebana , kwa sababu AYUNI alitaka amtambulishe mji unasemaje akamfungulia
Kiba akawa anatafuta sehemu akojoe kila sehemu wapo watu , alizunguka sana mwisho alipata chochoro kwa bahati mbaya alishuka na begi lake na wajanja wa mjini wakajua wakuja huyu " mgeni wa mji" anamaliza kuachia kojo watu wakampora begi ikabidi aruke nao " kosa alilofanya ni kuwafuata yeye mgeni mjini"
Alikimbiza wewe wakati huo anazidi kuwa mbali na rafiki yake mwisho wale wajanja wakamzidi kete akawakosa kimoyo moyo akasema " kweli nipo mjini😂
Kiba akasema arudi alipo toka ndio akashtuka amepotea njia ya kurud amesahau , na hana simu rafiki yake nae anashanga kiba harudi akaendelea kusubiri ,akaanza kuzunguka akimuulizia kiba kwa maelezo ,jitihada zikagonga mwamba alisema tu kimoyo moyo
" wewe mtoto wa kiume pambana mpaka nitakapo kupata"
Kijijini walipata taarifa za kupotea kwa kiba waliumia sana , na hata hivyo AYUNI alitokea kumpenda sana ADA alimwekea vishawishi mwisho aliushinda moyo wa ADA
BAADA YA MIAKA 3
kiba anaonekana akiwa na mkokoteni umebeba madumu ya maji ya kutosha , anaingia nayo kwenye mgahawa na mgahawani hapo wanampokea kwa shangwe " kiba , kiba huyo , "
KIBA ALIVYO POTEA ALIPATA MSAADA KWA JAMAA MMOJA ALIYe KUWA ANAITWA RICHARD , RICHARD HUYO ALIKUWA NA MGAHAWA WAKE AMBAO NI WA KUHONGWA NA MKE WA MTU NA RICHARD PIA ANAMDOGO WAKE WA K**E ANAITWA REHEMA ,REHEMA PIA AZIPATANI NA KIBA
Kipa ananawa mikono na kuanza kutengeneza mishkaki , muda huo huo anakuja REHEMA na kuanza kufoka bila sababu ila kiba anampotezea kwa kukaa kimya
Somo kidogoo
" katika maisha jifunze kukaa kimya sababu kimya ndio jibu la kumpa mjinga , ukimjibu kwa kuongea unampa muongozo wa kukuingia, ndio maana umepewa masikio mawili mdomo mmoja , sikia sana ongea kidogo "
Tuendelee
Wakati kelele zikiendelea ghafla linakuja gari linasimama mbele ya mgahawa anashuka richi na kuagana na mwanamke mrembo ndan ya gari , yule mwanamke anamuona kiba anampungia mkono na kumsalimu " mambo kiba" kiba
Kiba anaigoma salamu kwa kukaa kimya,mwanamke anaona haitoshi anampigia simu kiba hapokea simu,mwanamke anawasha gari na kuondoka ,
Richi anafika anaingia mgahawani na anawapa hai wateja anaingia kaunta na kuangalia mauzo anakagua mazingira anamrudia kiba nje
"Vipi kiba " kiba kinyonge anajibu safi na kuiweka mishkaki vizuri ilikuwa tayari imeiva na kumuangalia usoni rafiki yake akamuuliza
" unajipenda rafiki yangu , unampenda mdogo wako , huyu mwanamke atakufikisha pabaya huyu mwanamke bwana wake anahela atakuja kukuuwa bure rafiki yangu "
Rich alikaa kimya muda Fulani na kumjibu
"Sikuelewi rafiki au unataka ukajimilikishe wewe hapa mjini ishi kwa akili , Mimi sio wewe mtu ambaye umemsubiri demu wako miaka miwili halafu unaenda kumchukua unaambiwa ameolewa yule mwanamke sio k**a ADA chali yangu nipo nae kwa miaka , sorry k**a nimekukwaza unakera ,muda wote jambo hilo tu"
KIBA alipo sikia ADA alikuwa mpole kweli ,muda huyo huyo wanasikia kelele mgahawa wa tatu REHEMA kakiwasha haswa kila dumu la maji , kiba anafika pale rehemu kashikwa roba na lijamaa huku likimkoromea , kiba alipata hasira sana
Waliwafuata na kuwaachanisha kwa nguvu akamwambia rehema tangulia akamwambia yule jamaa
" jamaa yangu usijione unamaanguvu sana Mimi sipigani kushindana , mimi napigana kutafuta heshima na weza nikakuuwa unajua nilipotea mimi , na sitaki nikuone ukimshika rehema wetu"
Rehem anaonekana akisikiliza kwa kuibia .
USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA